Swahili Service

ADUI ANAPOKUWA DANI TAYARI

WAEFESO 4:27; 17
YAKOBO 4:7

UTANGULIZI

Wakristo wengi wanakaa katika giza kuu ya kutofahamu juu ya adui wa nafsi zao. Hivyo adui anapata nafasi kuu kuingia na kukaa ndani yao. Biblia inasema “Wala msimpe Ibilisi Nafasi” Maanake ni rahisi sana mtu kumpa adui nafasi katika maisha yake. Ukimpa adui nafasi basi atakaa. Wengi wetu tunatafuta adui inje ya maisha yetu bali adui amekaa ndani “Mpigeni shetani naye atawakimbia” (Yakobo 4:7) maanake usipompiga shetani basi yeye atakaa. “Shetani asije akapata kutushinda kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake” (II Wakorintho 2:11) ikiwa hatujui binu za shetani, basi shetani atapata nafasi kubwa. Kizazi cha sasa kina kaa katika giza kiroho (Yohana 3:19) Sodoma na Gomora zimekuja nyumbani kupitia TV, nguvu za giza zimejaa kila mahali. Pengine mnajua sana nyimbo za sifa na ibada lakini maisha na style yako haionyeshi Kristo. Adui anapoingia ndani mambo yetu yanaenda mrama.
Hebu tuone:-
I. JE MAANA YAKE NINI KUMPA IBILISI NAFASI ?
1. wakati tumeipa dhambi nafasi ndani yetu. Hata dhambi ya kutazama (peeping acts of sin)
2. Wakati tunampa shetani nafsi ndani yetu kwa kule tunaenda (Hot head saloon, mer-maid hotel) utukufu wako unaweza kuibwa.
3. Wakati tunapokula katika meza ya ibilisi na mapepo, Zaidi wakati huu wa sherehe.

4. Wakati tuna mwacha shetani kubandilisha hati-ma yetu kupitia waganga na wasomao nyota. Hivyo uzuri wako unaibwa.
5. Tunaposhiriki usherati na usizi (Adultery & For-nication)
6. Tunapoishi katika hasira , uchungu na ghatha-bu.Hasira inaonyesha jinsi ulivyo, hasira ina-fupisha maisha, hasira ni silaha ya adui zako. Anaye kukasirisha ana kushinda. Adui anaona udhaifu wako ni hasira, basi atatumia hasira yako dhidi yako (Musa)
 Watu wa hasira nyingi ni wale watupu. Jinsi su-furia ilivyo na maji kidogo ndivyo inachemka upesi zaidi!!
7. Tunapo kataa msamaha kwa wengine ndivyo pepo za kuumiza (Tormentors) zitaongezeka ndani yako.
8. Tunapokaa na chuki ndivyo tunampa ibilisi nafasi. Chuki ni kama jinsi kuchoma nyumba yako hili kuua panya. Chuki ni kama mauji. Chuki ni fimbo ya kujichapa mwenyewe.
9. Tunapo chukua kile si chetu, yaani wizi, tunam-pa shetani nafasi. (Akani(Yoshua 7:1-6), Gehazi II Wafalme 5:20-27)
10. Kukaa na vitu vilivyo chukizo kwa Mungu nda-ni ya nyumba hau mwili wako.
11. Tunapotumia ulimi wetu mbaya ,hau tunapo ku-wa walafi.
12. Tunapoishi katika fadhaa. Tunapokimbia mbio zisizo zetu.
13. Tuna kaa na uchungu, na tunapofungua roho zetu kwa pepo, tunapozidi katika dhambi za nyumba ya baba zetu, tunapo chukua mambo ya Mungu mzaha, tunaingia vyama vya wenye dhambi.

II. JINSI YA KUPAMBANA NA ADUI ALIYE NDANI TAYARI.
Tubu dhambi zote, mchukie shetani na kazi zake .
Omba maombi ya kung’oa muguu ya ibilisi.
MWISHO
Maombi
1. Kila mgeni wa giza katika hekalu la maisha yangu, kufa sasa katika Jina La Yesu Kristo.
2. Kila mshale wa uchawi ndani ya mai-sha yangu , Kufa sasa Katika Jina La Yesu Kristo.
3. Kila uchawi wa mazingira yangu kufa katika Jina la Yesu Kristo.
4. Kila hatima yangu iliyo bandilishwa na shetani ninaidahi sasa katika Jina La Yesu.
5. Sasa ninang’oa miguu ya shetani kutoka kwa nyumba na maisha yangu Katika Jina la Yesu Kristo.

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *