Swahili Service

AHITHOFELI ALIPANGA, LAKINI MUNGU ALIPANGA VIGINE

SOMO:  II SAMWELI 16:20-17:21

UTANGULIZI

Mungu aliingilia kati mpango mbaya wa Ahithofeli na Absalomu kumshusha na kumwaribu mfalme Daudi. Mpango wao haukufaulu kamwe.   Kuna watu wanaokaa kama jinsi bomu. Hawa watu sura yao kawaida wanaongea na kutembea kawaida. Wanaudhuria kanisa an kusifu Mungu kawaida, lakini dani yao kuna shida kubwa. Hawataki kamwe kuongea maisha yao yaliopita. Hivyo lazima kuchunga sana. Hawa watu huwa walipata shinda kale hau waliumizwa sana na mtu lakini hawakupokea ushauri   kamili kutoka kwa Biblia, hivyo wanabebana na chuki na uchungu zaidi. Leo tunatazama watu wanne katika somo hili Ahithofeli, Daudi, Absalomu na Hushai. Ahithofeli alikuwa na chuki. Daudi alikuwa amemvuta Ahithofeli karibu sana na nyumba na ufalme wake. Ahithofeli alikuwa baba yake Bathsheba mke wa uria mhiti. Ahithofeli hakupendezwa na jinsi daudi alimfanya Uria, na jinsi alivunja ndoa ya    Bethsheba na Uria na kumuua Uria. Kila siku uwe macho sana na watu uliokosea kitambo. Ahithofeli alibeba uchungu wa kitambo juu ya mfalme Daudi hata ikawa Daudi alimtenda mema Ahithofeli bado alibeba chuki na uchungu kwa miaka mingi.

Hebu Tuone:-

I.  Kubeba Chuki Huleta Uchungu, Mwenye uchungu hawezi kuwa mtu mwema (Waebrania 12:15)

 • Ikiwa unachukia, basi wewe pia ni mtu wa uchungu.
 • Uchungu ina mizizi yake (Waebrania 12;15)
 • Uchungu unampeleka mtu mbali na neema ya Mungu.
 • Uchungu unampeleka mtu mbali na hatima (destiny ) yake , hivyo uchungu unaharibu hatima ya mtu.
 • Uchungu kama jinsi mizizi inajificha sana chini ya undogo wa maisha.
 • Uchungu ni dhambi inayo tawala maisha na nafsi (Bitter people don’t get better !!)

II.  Mtu Mwema Anaweza Kuwa Mtu Wa Chuki (2 Sam. 15:12)

 • Ahithofeli alikuwa mtu mzuri tena mtu wa ibada kwa Mungu.
 • Ahithofeli alimtolea Mungu dhabihu.
 • Ahithofeli alikuwa mtu wa ushauri mwema, ushauri wake ulikuwa kama ushauri wa Mungu (2 Sam.16:23)
 • Alikuwa mtu wa ushauri mkuu wa mfalme Daudi.
 • Ahithofeli alikuwa mtu mwaminifu, hivyo alipewa nafasi ya usemi mkuu kwa mfalme Daudi.
 • Ahithofeli alikuwa rafiki mkuu wa mfalme Daudi (Zaburi 41:9)
 • Lakini hata ingawa Ahithofeli alikuwa mwenye ibada, mshauri an rafiki wa mfalme, alikuwa mwenye chuki, uchungu, hasira na adui.

III.  Uchungu Unafunika Hekima na Akili

 • Huyu mtu wa hekima alikuwa anakulwa na chuki dani yake kwa miaka.
 • Ahithofeli alikuwa mnafiki sana (Mathayo 23, Waebrania 4:13)

IV.  Dhambi Inafungua Njia Kuu Yakupimwa Kiroho

 • Shetani anangojea mtu afungue njia kwa kuanguka katika dhambi.
 • Tunapoanguka katika dhambi, Mungu anatoa ulinzi wake dhidi yetu
 • Daudi alifanya dhambi na Bethsheba, alifungua mlango ya shinda, Amoni alimnajisi Tamari dada yake an Absalome akamuua Amoni.
 • Absalom naye akageuza uongozi wa Daudi.

V.  Shina la Uchungu ni Chuki

 • Ahithofeli alikuwa na mwana kwa jina Eliamu,. Eliamu alikuwa babake Bethsheba (2Sam 23:34)
 • Ahithofeli alimtumia Absalomu kulipiza kisasi.

VI.  Chuki Ndiyo Chanzo Cha Kulipiza Kisasi (2 Sam 16:21-23)

Ahithofeli alimshauri Absalomu ,mambo mawili

 1. Lala na wake wa baba yako juu ya paa ya nyumba pale pale Daudi alipolala na Bethsheba !! Mchana na mbele ya watu wa Israeli (2 Sam 12:11)
 2. Ahithofeli alimwomba Absalomu Askari 12,000 kupigana na mfalme Daudi.
 • Lakini Mungu alikuwa na mpango wake.

VII. Mungu Mshauri Mwema, Anao nguvu za kuvunja Mipango ya shetani juu ya Maisha Yako.

 • Kulikuwa na mtu kwa Jina Hushai (2 sam. 15:37)
 • Hushai alikuwa rafiki wa kweli kwa mfalme Daudi.
 • Absalomu alipokea ushauri wa Hushai (2 Sam 17:14)
 • Lakini Ahithofeli alikwenda kwake nyumbani na kujiua.
 • Chuki mwisho wake ni mauti.

MWISHO

 1. Je unaye rafiki wa kweli, hau Ahithofeli ndiye rafiki wako ?
 2. Mungu atainuka juu ya Adui zako wanaopanga mpango kwa siri juu yako.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *