Swahili Service

ASUBUHI YANGU NJOO

SOMO:  ZABURI 30:5

UTANGULIZI

Mungu wetu Jehova hajali ata iwe ni kuua , kuondoa, kufuta, kufangia hau kufanya chochote kile hili kutosheleza watoto wake. “Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, katika radhi yake mna uhai,. Huenda kilio huja kukaa usiku, lakini asubuhi huwa furaha “ (Zaburi 30:5) ‘For his anger endureth but a moment in his favour is life, weeping may endure for a night, but joy cometh in the morning”

I.  KUTOKA KWA KIFUNGU HIKI TUNAWEZA KUJIFUNZA MAMBO NANE:-

 1. Usiku na giza maanake kilio “Kilio huja kukaa usiku”
 • Pegine adui amekufanya kulia usiku.
 • Lakini ninakutangazia na kutoa unabii dhidi yako, kilio chako kimekoma sasa katika jina la Yesu.
 • Usiku ndiyo wakati wa adui kufanya kazi yake.
 • Usiku unatoa mazigira mema ya maovu, hivyo usiku ni kilio na manunguniko mengi hutokea.
 1. Asubuhi ni wakati wa furaha –Hivyo nakutolea unabii kwamba asubuhi yako imefika. Furaha yako adui aliyechukua, lazima kurudisha katika Jina la Yesu.
 2. Mungu Hakupanga kwamba usiku uweze kuendlea daima– Hivyo hali yako ya sasa si ya kudumu daima. “Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha”
 3. Kwa kila usiku kuna asubuhi yake. Ninaomba sasa Asubuhi yako ije katika Jina la Yesu.
 4. Adui yako hana neno la mwisho juu ya maisha yako.
 • Hakuna mtu aliye na neno la mwisho kwa maisha yako.
 • Hakuna hali ambayo ni ya kudumu daima.
 • Kunaye Mungu mbinguni– yuko juu ya vyote na wote.
 • Mungu pekee ndiye aliye na neno la mwisho juu ya maisha yako.
 • Mungu anaposema na iwe nuru– Ni nuru !!
 • Neon lake linatuliza kila hali kuinama.
 1. Nguvu zote za giza zinakimbia Asubuhi inapopambazuka. Hivyo kazi ya giza imepangiwa usiku pekee, asubuhi inapokuja , kazi za giza zinakuwa dhairi. Hivyo giza hupenda sana kukimbia.
 2. Ikiwa basi umekuwa katika kulia, tulia, kwasababu asubuhi yako imetokea.
 • Fahamu hivi , kilio hakitafanya adui asifanye kazi yake na pia kilio hakiwezi kuleta mkono wa Mungu.
 • Kilio ni ishara ya kukosa Imani, kilio kinamsaidia adui.
 1. Kuvunjika moyo na kukata tamaa kunaleta mauti – Imani inaona njia wazi (Yoshua 10:11-13)
 • Imani inasimamisha jua na mwezi mbinguni.
 • Hivyo Mungu yuko tayari kufanya chochote kwa ajili ya watoto wake.
 • Mchana ukawa mrefu kuliko kawaida, lakini giza ikawa mrefu zaidi upande ule mwingine.
 • Kule Misri, wamisri walipopata giza, palikuwa nuru kwa wana wa Israeli (Soma Isaya 43:3-4)
 • “Kilio huenda kikaja usiku, lakini furaha huja Asubuhi”.
 • Kufa moyo kunaona giza, lakini Imani inaona asubuhi.

II.  JE ASUBUHI YANGU ITAKUJAJE ?

 1. Mtazame Yesu Kristo pekee- Usitazame hali yako.
 2. Mungu ataenda mbali sana, kuwaita watakao kusaidia.
 3. Wasaidizi wako hawatatulia mpaka wakusaidie wewe.
 4. Weka mbali sana roho ya kuvunjika moyo na kukata tamaa (Yohana 14) Okoka ikiwa bado.
 5. Anza vita na kila roho na nguvu ambazo hazitaki ufanisi wako (Dada 39 alikuwa amefungiwa ndoa, mama, ndugu na baba waliaga)

 

 

III.  MAOMBI

 • Kila nguvu za giza upande wa mama, zinazo fanya nisiendelee kufa sasa– katika Jina La Yesu.
 • Kila roho na nguvu katika nyumba ya babangu inao sema nitakufa katika hali duni, kufa sasa katika jina la Yesu.
 • Soma Isaya 8:9-10, wacha maadui zako waoongee lakini watavujwa vipande vipande !!
 • Angalia maisha yako, ni kitu gani shetani amekunyang’anya– Amua ndani yako kwamba unavitaka sasa. Omba Mungu.

 

MWISHO

Maombi

 • Wasaidizi wangu, njoo kwangu kwa njia ya moto katika Jina la Yesu Kristo
 • Kila ratiba ya umasikini iliyopangwa juu yangu, chomeka sasa katika jina la Yesu.
 • Kila ukuta wa ukoo, uliojengwa dhidi ya utukufu wangu, vunjika sasa katika jina la Yesu.
 • Kila ndege wa giza anayekesha kwa ajili yangu, kufa sasa, katika jina La Yesu.
 • Bwana wangu ongeza mwendo wangu hili nifike kwa shabaha zangu, katika Jina La Yesu.
 • Moto na ngurumo za Mungu inuka juu ya adui za maisha yangu, katika Jina La Yesu.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *