Swahili Service UKOMBOZI

BADILIKA– UKAINUKE

JEREMIAH 48:11

UTANGULIZI

Watu wengi wanahitaji ujumbe huu zaidi. Hapa twaona kwamba Moabu alikuwa na shida nyingi. Kwanza Moabu alipenda maisha ya starehe, Pili Moabu alitulia juu ya sira zake, Tatu Moabu hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine.

Moabu hakwenda kufungwa (captivity) kwa hivyo ladha yake anakaa nayo, harufu yake haikubadilika. Moabu alikataa kubadilika hivyo moabu alinuka. Kila anayefanya kazi na Yesu lazima kubadilika. Mlevi anapookoka maisha yanabadilika. Maisha ni kubadilika. Watu wengi wanataka kukaa bila kubadilisha mawazo na tabia. Watu wa Biblia mara kwa mara walitembea mbali, Musa Ibrahimu, Yakobo, Yeremia. Hivi leo amua kubadilika. Hivyo marafiki wengine lazima kuwaacha, mawazo yako, tabia na mazoea, marafiki wengine wamekurudisha nyuma, tamaduni zingine zimekuwa duni, hata mbegu ni lazima kuanguka kwa udongo na kufa ili uweze kuzaa sana. Maji yakikaa mahali pamoja yanalete umbu. Kanuni ya kubadilika ni kanuni ya nguvu.

I.  VITA VYA KIROHO VINALETA MABADILIKO

 • Ni pamoja na kupingana na shetani na pepo wachafu.
 • Ni kuchukua uongozi wa akili na mawazo yako.
 • Ni kuchukua hatua kwamba mambo mengine utayaacha kabisa.
 • Ni kusulubisha mwili na matendo yake.
 • Vitu na shetani hutengemea sana jinsi unahusiana na shetani( Wakolosai 3:5) lazima kuzifia dhambi na matendo ya mwili.
 • Maiti haijaribiwi na shetani, maana maiti haijui kama kuna mtu anamsema, maiti haina matusi kwa watu, maiti hajui usharati na ulevi.
 • Mtu akikufa mwili, shetani hawezi kuendelea kukaa dani yake.
 • Hivyo lazima kuvunjika roho zetu.

II.  MUNGU ANAPOFUNZA NJIA– ANADAI MABADILIKO

 • Adamu alifungiwa njia.
 • Balaamu alifungiwa njia.
 • Yona alifungiwa njia.

Mpango wa Mungu ni kutubadilisha tukae kama Yesu  Kristo. (Warumi 12:1-2)

 • Mungu si kama fundi wa nguo, kurekebisha nguo mpaka kipimo (size) ya mtu.
 • Watu wengi hawapendi mabandiliko na kumbe mabadiliko ndio njia ya raha na amani.

III. SABABU YA MABADILIKO DANI YA MAISHA YETU.

 1. Maendeleo kiroho (Divine advancement)
 2. Kupanuliwa na Mungu.
 3. Kuogezewa na Mungu.
 4. Kupewa hatua mpya na muelekeo mpya.
 5. Kupewa kazi mpya na Mungu.

Kukataa kubadilika na kunuka kama moabu.

IV.  NANI ANAHITAJI KUBADILIKA ?

 • Kama maisha yako niyakupungukiwa.
 • Kama maisha yako niya kusubuliwa,
 • Kama umekosa mwelekeo.
 • Kama umekufa moyo.

V.   BASI TUFANYEJE KUBADILIKA ?

 • Fungua maisha yako kwa Roho Mtakatifu.
 • Fungua shamba la moyo wako kwa Mungu.
 • Kila sehemu dani ya maisha yako inayohitaji msaada wa Mungu lazima kusalimishwa kwake kikamilifu.
 • Jifundishe kusikiza kuliko kunena,badili ratiba ya maombi, kusoma Biblia na jinsi unavyo wachukua watu, kata kusikiza masengenyo.

MWISHO

Omba:

 1. Ee Bwana, kila sehemu inayoitaji mabadiliko ndani yangu, badilisha, Katika Jina la Yesu.
 2. Kila urithi wangu ndani ya Yesu Kristo naomba unifikie sasa katika Jina La Yesu.
 3. Kila Jambo ndani yangu inaofungia mkono wa Mungu kuja kwangu, Ishindwe sasa, Katika Jina La Yesu.
 4. Kila kizuizi cha kupenya kwangu, vunjika katika jina la Yesu.
 5. Bwana wangu, nipanulie mpaka na kunizindishia Baraka zako, katika Jina la Yesu Kristo.

 

 

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *