Series Swahili Service WANAWAKE SABA WENYE IMANI YA BIBLIA

ESTA– MWANAMKE ALIYE SEMA NDIO KWA MUNGU

ESTA 2:5 ; 3:13

UTANGULIZI

Esta aliishi kwa Imani. Maisha yake Esta inatuonyesha kwamba Mungu anaye mpango na mahali na nafasi kwa kila mmoja wetu. Kila Mtu anayo      Historia, lakini tunawakumbuka wale walio tembea katika Imani wakawa wenye kuunda historia.       Historia ya Esta inatufundisha kwamba Mungu anachangia pakubwa sana katika historia maana historia ni kazi yake ndani yetu (HIS– STORY). Hivyo Mungu huwatumia watu wa kawaida kutengeneza historia.

Esta alitumiwa na Mungu kumbandili historia ya taifa nzima. Lakini ni kwa sababu Esta alisema ndiyo kwa Mungu. Kama Esta angesema La kwa mpango wa Mungu, Mungu angalimtumia mtu mwingine, lakini naye Esta hangelijulikana. Esta alikuwa na Imani inayokata shauri. Jina lake ya   kiyahudi aliitwa Hadassa. Jina Esta maanake Nyota (Star). Nyota hungara gizani. Binamu wake   Modekai alikuwa mtumishi wa mfalme pale Shushani Ngomeni. Malkia Vashti alikataa amri ya mfalme, hivyo akamtalaki. Hamani naye alikuwa waziri mkuu, mtu wa ukoo wa Amaleki, taifa lililo wachukia wayahudi sana (I Sam.15:1-3). Hata ingawa Esta alikuwa yatima na mtumwa, neema ya Mungu na kibali mbele ya watu wote na zaidi sana Hegai mkuu na msimamizi wa nyumba ya wanawake– Yaani mwenye kuwalinda wanawake wote wa mfalme. Hebu tuone kanuni tatu za kutembea katika Imani:-

I.  JIFUNDISHE WAKATI WA KUNYAMAZA (LEARN WHEN TO SHUT UP)

 • Jifundishe kuwaelewa watu– Elewa na yale watu wanawaza.
 • Kunyamaza kunakusaidia kuelewa na mawazo ya watu unakoishi.
 • Ikiwa utakuwa mtu anayetengeza historia dunia hii lazima kujua wakati wa kunyamaza na kusikiza watu.
 • Esta alimsikiza sana Mordekai mjomba wake na Esta alitulia na kusikiza.
 • Esta alikataa kufichua kabila, utaifa na jamii yake kwa wangeni.
 • Mordekai alikuwa amemshauri hivyo, kwa maana si kila mtu ana haki ya kukufahamu (Esta 2:10)
 • Usiwaambie watu wewe ni nani, lakini waambie kinyume.
 • Kule kunyamaza kwa Esta kulihifadhi maisha yake na kumpa uwepo mbele ya mfalme.
 • Hivyo kunyamaza na kusikiza kutakupatia nafasi katika maisha na ulimwengu wa mwezako.
 • Mtu hawezi kuwasaidia watu mpaka apate kuwaelewa hili aweze kuwa na usemi katika maisha yao na kumbandili historia ya maisha yao (Mithali 18:2)
 • Tusiwe watu wanao funga akili zao na kufungua midomo yao.
 • Wenye kutengeza historia ni watu wenye kusikiliza watu, ni wale wanao jifanya kuwa wanafunzi wa watu na hali yao (Mithali 11:12)
 • Hivyo ikiwa utakuwa mtu atakaye saida watu wengine na kungeuza hatima na historia yao kimya na sikiza watu.

II.  JIFUNZE WAKATI WA KUONGEA.

 • Dr. Dietrich Bonhoeffer alikuwa mhubiri wa Lutheran Church Ujerumani (German) wakati wa Hitler. DB alikuwa kunyume kwa Hitler mpaka kuusika katika mpango wa mauaji yake Hitler. DB alikamatwa na Nazis 1943 na kauliwa 1945, mwisho wa vita vya II. Alipoanza kuongea juu ya haki za watu.
 • Esta alimwambia mfalme “mtesi na adui yetu ni mtu huyu Hamani” (7:6-7)
 • Hatuwezi kamwe kunyamaza juu ya Imani yetu.
 • Kristo alishauri juu ya kutangaza Imani yetu (Marko 8:38)
 • Mtume Paulo naye ametushauri (Warumi 1:16-17)
 • Kuongea kunaweza kuleta shida na mauti (II Tim.1:8)
 • Ni lazima kuwa tayari kutangaza (I Peter 3:15)
 • Tunaongea lini?
 1. Tunapoulizwa kuongea , Mfalme na Mordekai walimwomba Esta kunena.
 2. Wakati wa kulinda maisha ya watu wetu na haki zao.
 3. Wakati wa kueneza ufalme wa Mungu.

III. JIFUNDISHE KUMWONA MUNGU

 • Esta alifahamu kwa kuwa malkia ulikuwa ni mpango wa Mungu (4:14)
 • Mungu anao mpango wa jabu kwa miasha yako, nyumbani, kazini, shulani, kanisani, duniani (I Wakorintho 7:17, Mithali 16:4)
 • Mungu yuko kazini, Mungu Mwana naye yuko kazini, Mungu Roho yuko kazini, sisi pia (Yohana 5:17)

MWISHO

 • Esta aliishi kwa Imani katika inchi ya kigeni.
 • Esta alifanya historia, mpaka leo wana wa Israeli wanasherekea siku kuu ya Purim.
 • Musa naye kama Esta aliamua kujitambulisha na watu wa Mungu (Waebrania 11:24-29)

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *