MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANI Swahili Service

IMANI NDIO USHINDI (FAITH IS THE VICTORY) : WAEBRANIA 11:32-40

UTANGULIZI

Tunaishi katika kizazi kinacho amini kwamba kushinda ndio mambo yote. Hata kanisa limeamini Imani ya kweli lazima ushindi na maendeleo ya binafsi, Injili ya “Afya na Utajiri”. (Health and wealth gospel) lime tujulisha ikiwa wewe si tajiri na mwenye afya nzuri umekosa Imani. Lakini sivyo kulingana na Biblia. Leo mwandishi wa Waebrania anatujulisha kwamba Imani kiini chake ni mambo mawili. Imani ndio ushindi lakini pia Imani ni kustahimili katika shida, mateso, dhihaka na mauti.

Hebu tujifunze:-

I. KWANZA, USHINDI MKUU WA IMANI (Waebrania 11:32-35)

 • Kwanza, mwandishi wa Waebrania ameona wakati hautoshi kuleta habari zote !! (V.32)
 • Anataja watu sita wenye Imani kuu.
 • Hawa ni Gideoni, Baraka, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samweli na Manabii.
 • Hawa ni watu kutoka wakati wa waamuzi mpaka wakati wa wafalme na manabii.
 • Hawa watu waliotajwa walimwishia Mungu nyakati ngumu duniani.
 1. Gideoni pamoja na watu mia tatu (300) walishida vita dhidi ya jeshi la midia. (Waamuzi 7:7-25)
 2. Baraka pamoja na Debora walishida vita juu ya Wakanaani (Waamuzi 4:8-10)
 3. Samsoni pamoja na udhaifu wake alishida vita juu ya wafilisti (Waamuzi 13:1-16:3`)
 4. Jeftha pamoja na nadhiri yake ya ujinga alishida vita juu ya Waamoni ( Waamuzi 11:1-12 ;7)
 5. Daudi aliishi kwa Imani pamoja na makosa na dhambi zake. Mungu alishuhudia kwamba Daudi aliutafuta uso wake Zaidi ya wote.
 6. Samweli kutoka utotoni alimtumikia Mungu na kuwaamua Israeli maisha yake yote.
 7. Manabii walimtumikia Mungu kwa furaha na ujasiri mkuu. (V.33-35)
 • Hawa walipata ushindi kisiasa, waliongoza vyema serikalini,-wakapata ahadi za Mungu.
 • Wengine walipata ukombozi (Danieli 6:23)
 • Wengine walizima moto (Danieli 3:16-30)
 • Wengine kama Eliya, Elisha na Yeremia walipona makali ya upanga.

II.  PILI, KUSTAHIMILI KWA IMANI. (Waebrania 11:35-40)

 • Lakini wengine, waliumizwa vibaya hata kuuwawa.
 • Hawa hakubali ukombozi iliwapate ufufuo ulio bora.
 • Hawa kwa aimani walipenda ufufuo wa Kristo, ufufuo wa utukufu wa Mbinguni, Lakini ufufuo wapate kufa tena !!. Kama jinsi Lazaro. (V.35)
 • Wengine walijaribiwa kwa dhihaka, mapigo, mafungo na kutiwa gerezani.
 • Wengine walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno N.k.
 • Hawa wengi hivyo hawakupata zile ahadi, walistahimili kumwona Mungu wao !!
 • Hawa wanaume kwa wanawake wa Imani hawakukombolewa kutoka kwa shida zao, lakini Mungu anapogeza Imani yao.
 • Imani ya kustahimili ni kuu kuliko Imani ya kushida vita zako zote (Danieli 3:16-18)
 • Katika kuokoa hau kustahamilisha– Ukuu wa Mungu unaonekana.
 • Mungu asipookoa yeye anadumisha kwa ustahimilifu.
 • Katika Imani hizi mbili, wote waliona kwamba katika mambo yote, ushindi hau kustahimili.
 • Mungu ni mwema zaidi kuliko vyote.
 • Kama ni kupata yote, hau kupoteza yote Imani ni kusema “Mungu ni bora Zaidi”

 

MWISHO

¨ V.40, Hadithi ya Imani haiwezi kukamilishwa bila wewe na mimi !! Mungu anaendelea kuandika safari ya Imani yako !!

¨ Maisha ya Imani si ya “wachache waliochanguliwa”

¨ Maisha ya Imani yanawezekana kwa kila aminiye katika kila hali ya maisha.

¨ “Imani ndio ushindi”

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *