Swahili Service

INUKA, UANGAZE

ISAYA 6:1-5

UTANGULIZI

Jumapili iliyopita tulinena juu ya Kibali-ngao ya wenye haki (Zaburi 5:12). Leo hii  Bwana anasema inuka, ondoka, uangaze kwa maana nuru yako imekuja na utukufu wa Bwana umekuzukia. Ni mapenzi ya Mungu wana wake wote kuondoka na kuinuka kufikia hatua ya juu zaidi katika eneo zote za maisha na kuonyesha sababu na utukufu wake Mungu hili kuvuta wengine kwa ufalme wa Mungu.

Hebu tuone mambo manne Dhahiri katika kifungu hiki:-

I.  MWITO WA KUINUKA NA KUANGAZA.

 • Kwanza kuna amri ya Mungu kuinuka, kuondoka na kuangaza.
 • Si mapenzi yake wanaye wakae mahali pamoja bila kwenda mbele.
 • Mapenzi ya Bwana ni kila anaye mwamini kuinuka, kuondoka na kuangaza, huku tukienda mbele katika kila eneo katika maisha yetu.
 • Hebu tuone jinsi hawa watu walikuwa kabla ya kuambiwa wainuke, waondoke na kuangaza.
 1. Walikuwa katika hali ya kuanguka (Mika 7:8)
 • Nikawaida kuanguka katika dhambi, makossa na udhaifu.
 • Ni mapenzi ya Bwana kukuinua na kukusimamisha.
 • Kuanguka kwako si mwisho wako. Bwana amekupangia hali yako ya mwisho (Final state)
 1. Walikuwa katika hali ya mauti (Ezekieli 37:10)
 • Bwana yuko na mpango kukuinua kutoka hali ya mauti ya kiroho na kila kitu kilicho kufa ndani yako.
 • Bwana yuko na mpango wa kukuinua na kukupa uhai. Hivyo nina tabiri uhai kwako.
 • Chochote kilicho kufa ndani ya mwili wako kikaishi sasa katika jina la Kristo.
 1. Walikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa (Matendo 9:6)
 • Pengine umechanganyikiwa hujui ufanyeje’
 • Shetani anapenda sana ukae katika kuchanganyikiwa– Roho iliyo changanyikiwa ni roho mateka.
 1. Walikuwa katika hali ya ukiwa (Idle) Matendo 9:10-17
 2. Walikuwa katika usingizi mwingi (Matendo 12:1-7)
 • Kanisa lilipolala kiroho, Herode aliwaingilia,
 • Walipoinuka na kuomba, Petro alifunguliwa.
 1. Walikuwa katika hofu na hali ya kutokuhusika kama jinsi Musa, Gideoni, Jonah, Joshua.
 2. Walikuwa katika hali ya uzembe. Tusipoinuka hatuwezi kuangaza.

II.  UWEZO WAKO KUINUKA NA KUANGAZA

 • Nuru yako imekuja na utukufu wa Mungu huko juu yako.
 • Yesu Krsito anaangaza juu yako (Zekaria 4:6)
 • Vijana na wana wa Skeva walijaribu kuangaza bila Yesu wakaona shida.

III. SABABU YA KUINUKA NA KUANGAZA

Wengi watamjia Yesu Kristo,

 1. Giza inaifunika dunia yote (I Yohana 2:15-17)
 2. Giza inafunika watu– Dunia imejaa watu wengi (Zaburi 1:1-3).

UNABII UNAO TAJWA JUU YA KUINUKA NA KUANGAZA KWAKO.

 1. Mataifa yatakuja kwa nuru.
 2. Wafalme watakuja kwa mwanga wako.
 3. Wana wako watakuja kutoka mbali
 • Wale walioibwa, walioharibiwa, waliopotea, waliocheleweshwa, watakuja kwako.
 1. Mungu atakupanulia mpaka wako (v.5-6)
 2. Utajiri wa mataifa utakujia mara moja

 

MWISHO

 • Mungu anasema kwako, inuka, ondoka ukaangaze
 • Mungu anasema Baraka zako zitakuwa nyingi sana utakapo inuka.
 • Makusudi ya Mungu kwako yatatimia, Baraka zake zote zitakujia.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *