SAMWELI Swahili Service

KAMA SI PENINA

SOMO: I SAMWELI 1:1-10.

UTANGULIZI

Matusi ya Penina kwa Hanna yalikuwa mpango wa Mungu kuelekeza Hanna kwa ushindi na hatima yake. Hivyo Hanna mshukuru Penina katika maisha yako. Jumapili ya jana tuliona kwamba Hanna hakuwa na binu za kutazama kando, lakini alipotazama Juu na Mbele, Bwana alimjalia na kuyajibu maombi ya moyo wake. Samweli wa Kwanza inatueleza kisa cha Elkana na jamii yake. Elkana alikuwa na wake wawili. Penina maana yake ni Mrembo (beautiful). Hanna maana ya jina ni Kibali hau Neema. Tunapoishi katika njia ya haki, hata ingawa kuna watu wengi warembo kukuliko, hata wajalipo kuwa na nguo zuri kuliko wewe, Neema na Kibali cha Mungu itakuelekeza kwa hatima yako katika Jina la Yesu. Penina alikuwa na watoto waume na wake. Hanna alikuwa akitafuta mtoto moja tu. Tunafanyaje wakati Adui zetu wanafanikiwa Zaidi kuliko sisi ? Kuchelewa si kunyimwa !!

Hebu tuone masomo kadha:-

 1. Somo 1: TUMIA HISIA ZAKO, LAKINI HUSIWACHE HISIA ZAKO KUKUONGOZA.
 • Elkana na jamii yake walikuwa watumishi wa Bwana.
 • Jamii ya Elkana pamoja na kutoka dani mbali na Shilo – Kila mwaka walikwea kwenda Shilo kuabudu Mungu – Usiwache umbali ukukoseshe Ibada.
 • Pale Shilo walikuwa na Eli na wanake –Wana wa Eli walikuwa wabaya,-Lakini umbaya wao haukuwakosesha Ibada.
 • Usikose Ibada kwa sababu ya mtu fulani, lakini mwadame Mungu –Mungu huwapa dhawabu wote wamtafutao (Waebrania 11:6)
 • Hanna alijua kwamba ufalme wa Mungu si kula na kunywa, lakini Haki, Amani na Furaha katika Roho Mtakatifu (Warumi 14:17)
 • Hanna alifahamu kwamba mapenzi ya mume yana kikomo chake (Isaya 40:6-8)
 • Hanna alijua kwamba Mapenzi ya Mungu hailinganishwi (Zaburi 125:1)
 • Hanna alijua kwamba hata awe na mume anayempenda – Mume hawezi kuelewa na uchungu wa moyo wake.
 • Hanna alijitenga na mume na jamii ili kumwomba Mungu.
 • Hanna alijua umuhimu wa kujitenga na mume na jamii na adui zake.

II. Somo 2: KUFUNGWA TUMBO SI UTASA

 • Utasa na kufungwa tumbo ni tofauti.
 • Shida ya kwanza ya Penina ni kufikiri Hanna alikuwa tasa. Kuna watu wanafikiri wewe ni tasa.
 • Shida ya pili ya Penina ni kufikiri Hanna atavunjika Roho na kukata tamaa.
 • Hivyo kuchelewa kupata mali, ukombozi, nyumba,Utasa si kunyimwa na Mungu.

III. Somo 3: MATUSI YA PENINA YALIPANGWA NA MUNGU.

 • Penina aliona kuwa yupo katika hatua ya juu Zaidi.
 • Kuna watu wanaona wamekupita kwa mbali.
 • Lakini kumbuka, kukimbia mbio zako mwenyewe.
 • Mungu atakuzindisha katika jina La Yesu Kristo.
 • Hanna alikataa kujibu Penina. Hezekia alikataa kumjibu Sennacheribu (Isa.36:21)

IV.  Somo 4: MATUSI YA PENINA YALIMPELEKA HANNA KUOMBA.

 • Hanna alikwea na kumwomba Mungu (I Sam.1:9-10)
 • Maombi ya Hanna yalikuwa na lengo kamili– Mwana wa Kiume.

 

 

V.  Somo 5: KUFUNGWA TUMBO YA HANNA KULIKUWA KWA MUDA NA KWA SABABU.

 • Mungu anafunga mlango kwa sababu yake. (I Wakorintho 16:9)
 • Mungu anataka kwanza kuwafurusha Adui zako.
 • Samweli alibarikiwa zaidi kuliko watoto wa Penina (I Sam.2:26, Luka 2:52)
 • Mungu alimtumia Samweli, lakini watoto wa Penina hata Majina yao hayajulikani.
 • Kama si Penina, Hanna angalikufa mbila kujulikana. Tumshukuru Mungu kwa Penina ndani ya maisha yetu !!

 

 

MWISHO

¨ Nani atakuwa na kicheko cha mwisho– Hanna.

¨ Nani atawacheka Adui zake– Hanna.

¨ Nani tunayehubiri leo– Hanna.

¨ Penina alikwisha hivyo, Hanna hajakwisha hata hivi leo. (Isaya 41:11-12, 50:8-9)

¨ Je umecheleweshwa, Je mlango wako umefungwa ? Mungu atafungua tumbo lako katika Jina La Yesu.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

2 thoughts on “KAMA SI PENINA”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *