Swahili Service

KIBALI– NGAO YA WENYE HAKI

ZABURI  5:12

UTANGULIZI

  Kitu kimoja kinachoweka wakristo wengi katika utumwa ni kutofahamu haki. Mtu anapookoka Mungu anamhamisha kutoka giza na kumweka kuwa kiumbe kipya. Mtu huyu anaingia katika    ufalme wa Mungu na kuwa Mwana wa Mungu na Hivyo mrithui wa Mungu pamoja na Kristo Yesu. Mtu aliyeokoka amekuwa mtoto wa Mungu, hivyo uhusiano mpya upo, hivyo kila mwana wa Mungu anapata haki na uhuru wa kuwa mwana. Katika uhusiano huu mpya mwenye haki anapata kibali kwa Mungu. Mungu yuko tayari kubariki kila mwenye haki na pia kumlinda kupitia kibali chake. Kibali cha Mungu kinapokuwa juu ya Mtu, Mtu huyo atalindwa na  upizani wowote wa mwanadamu. (Daniel 1:9). Baadaye, Daniel alipandishwa cheo hadi waziri mkuu katika inchi ya kigeni.

Hebu tujifunze:-

I.  MAANA YA KIBALI CHA MUNGU

 1. Wakati mtu anachaguliwa kwa jambo fulani kutoka kwa watu wengi, wote wanahitimu.
 • Esta alichanguliwa katika wengi waliohitimu kuwa malkia (Esta 2:15-17)
 1. Mtu anapochaguliwa kwa nafasi yenye hajahitimu katika wengi walio na ujuzi zaidi kuliko yeye. Daudi alikuwa ndiye mdogo zaidi katika nyumba ya mzee Yese. Mungu aliwakataa ndugu zake Daudi. (I Samweli 16:11-13)
 2. Mtu anapoutafuta uso wa Mungu katika maombi anapojimbiwa maombi yake (Yabezi-I Nyakati 4:9-10)
 3. Wakati msaada unapatikana katika wakati na mahali pasipo tarajiwa kama jinsi pale Bethsaida (Yohana 5:1-15)
 4. Mtu anapoitwa na Mungu kwa kazi kuu bila kutarajia kama jinsi Paulo (Matendo 9:1-6)
 5. Wakati mtu anaongozwa kwa kitendo kidogo kupata matokeo makuu, kama jinsi Petro na wavuvi wezake (Luka 5:1-11)
 6. Mtu anapokea huruma kutoka kwa wengine kama jinsi Yusufu (Mwanzo 39:1-6)
 • Kibali cha Mungu kinafanya mambo ya ajabu, Kibali kilimpata Musa jangwani, Daudi alikuwa na kondoo za babaye, kilimpatia Sauli Tarsus.
 • Kibali cha Mungu kinakuchangua kutoka kw a wengi kupata miujiza na wokovu (Marko 10:46-52). Batomayo alikuwa njiani pale Yeriko. Daudi alikuwa akidharauliwa na ndungu zake.

II.   MWELEKEO WA KIBALI CHA MUNGU.

 1. Kibali cha uponyaji- (Yohana 5:2-9), miaka 38-katikati ya wengi.
 • Naamani (2 Wafalme 5:1-14) Kristo alisema kulikuwa na wenye ukoma wengi, Samaria wakati wa Elisha– Naamani pekee alipata kibali.
 1. Kibali cha mali na vitu. (Luka 5:1-7)
 • Mungu anapochangua kukubariki na vitu, vitakuja.
 1. Kibali cha ndoa yako na jamii (I Samweli 1:9-20, Mithali 18:22) utapata mke, mme na watoto.
 2. Kibali cha akili na hekima (Danieli 2:20-22, Yakobo 1:3)
 3. Kibali katika huduma– Milango inafunguliwa, unahubiri kidogo na watu wanaokoka.
 4. Kibali katika eneo zote za maisha.
 • Yusufu hakupata ugonjwa maisha yake yote.
 • Yusufu alikuwa na Mali Zaidi (Mwanzo 45:4-13)
 • Yusufu alibarikiwa na akili na hekima ya ajabu (Mwanzo 41:39)
 • Yusufu alibarikiwa kijamii (Mwanzo 48:8-20)- Hata mke alipewa free.
 • Yusufu chochote alichofanya kilifaulu na kubarikiwa (Mwanzo 39:21-23)

 

 

III. KIBALI KINAPO HARIBIKA.

 1. Kibali cha Mungu kinaharibika kwa kukosa utii.– Sauli (I Sam.15:19-24)
 2. Kibali cha Mungu kinaharibiwa na dhambi ya usherati na tamaa za mwili (Waamuzi 16:18-21)
 3. Kibali cha Mungu kinaharibiwa na dhambi ya kiburi, shetani, Ibilisi (Isaya 14)
 4. Kibali cha Mungu kinaharibiwa na dhambi ya ulafi na ugumu wa kumtolea Mungu. ( II Wakorintho 9:6-15, Malaki 3:8-12).
 5. Kukosa uaminifu katika kazi ya Mungu.
 6. Kupanda mbegu ya uovu (Wagalatia 6:7-8, Waamuzi 1:5-7) Adonibezeki.
 7. Kukosa maombi– Esta, Nehemia waliomba

 

MWISHO

 • Kibali cha Mungu kinaleta Baraka zake, Hivyo kinapandisha juu (Mwanzo 39:21), Kinarudisha chochote shetani na adui aliiba (Ex.3:21) Kinaongeza mali (Kumbu.33:23)
 • Kibali cha Mungu hubandilisha mambo ( Esta 5:8, 8:5)
 • Kibali cha Mungu kinakupigania vita zote (Zaburi 44:3-8)
 • Gharama ya kibali cha Mungu ni kukaa katika haki na utakatifu. Hizi mbili huja kwa kuokoka na kudumu katika Bwana na neno lake.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *