MITUME WA YESU KRISTO Swahili Service

MAMA YAO ALIPENDA WAWE KAMA KRISTO-YAKOBO

SOMO: 

MATHAYO 20:17-28,MARKO 10:35-45

UTANGULIZI

Wanadamu wanapenda sana uongozi, mamlaka na uwezo. Mke wa Zebedayo, hau mama yao Yakobo na Yohana alipenda sana wanawe wapate mahali pa uongozi na mamlaka, upande we kuume na kushoto kwa Yesu Kristo na ufalme wake. Pia na wao Yakobo na Yohana walipenda sana wakajiulizia wenyewe.(Marko 10:35-45). Watu wanapenda sana mamlaka, uongozi, uwezo na cheo.

Lakini, Je, Kuna kinyume cha mamlaka, uongozi, cheo na madaraka ? Ndio:-

 1. ISHI MAISHA YA KAWAIDA– SI KUJIONYESHA.(Mathayo 20:20-21)
 • Mama Zebedayo alikuwa moja ya wanawake wengi walio jitoa kabisa kumtumikia Yesu Kristo na Huduma yake.
 • Alimfuata Yesu Kristo kutoka Galilaya kuhudumu (Matt.27:55-56)
 • Alijua Sasa ni wakati wa mwisho, na ni wakati bora Zaidi kumwomba Kristo, juu ya wanawe.
 • Mama Zebedayo alikuwa mama hodari, mama kiongozi na mama wakujivunia!
 • Mama Zebedayo pia aliona kweli wanawe, yaani Yakobo, Yohaha na Petro walikuwa karibu Zaidi na Yesu Kristo, hivyo, Petro alikuwa kikwazo kwa mpango wake.
 • Jamii ya Zebedayo ilichangia pakubwa Zaidi katika huduma ya Kristo– Watu watatu !!
 • Mama Zebedayo alitaka sana Kristo arudishe mkono !!
 • Hivyo, mama Zebedayo alishujudu mbele ya Kristo na kuomba jambo juu ya wanawe.
 • Ndiposa, wanafunzi wale wengine walikasirika sana!!
 • Kristo aliwaeleza gharama ya mamlaka, lakini wao walikuwa tayari kulipa gharama hizo !!
 1. ISHI MAISHA YA KUKATAA UBINAFSI– SI MAISHA YA KUSHIDANA (Mathayo 20:22-24)
 • Baba yangu alikuwa akisema “Kula chakula bila kujua gharama yake”.
 • Yakobo ndiye Mtume wa kwanza kuuliwa kwa upanga kwa mkono wa Herode. (Matendo 12:1-2)
 • Wanafunzi kumi (10) waliwachukia sana Yakobo na Yohana.
 • Yakobo na Yohana walipoulizwa kama walikuwa tayari kulipa gharama za mamlaka, wote pamoja walisema ndio!!

III. ISHI MAISHA YA KUTUMIKA NA KUHUDUMU– SI MAISHA YA UKUBWA. (Mathayo 20:25-28)

 • Kikombe alichonena Kristo ni kikombe cha mateso na kutenganishwa na Mungu Baba yake.
 • Kristo alituita tusipiganie ukubwa, mamlaka na vyeo.
 • Ni lazima tusiwe kama wakuu wa mataifa wanao watawala watu wao kwa nguvu na kuwatumikisha.
 • Yesu Kristo alikuwa tofauiti na watu wa mataifa. Alitumika na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi (v.28)
 • Wanafunzi wa Kristo walipenda kuwa mameneja !! Kristo aliwapa huduma, walipenda heshima, Kristo aliwapa unyenyekevu.
 • Wanafunzi walipenda ukuu, Kristo aliwapa utumishi.
 • Wanafunzi walipenda utukufu, Kristo aliwapa wema.
 • Anayetaka kuwa Mkubwa kwenu na awe mtumishi wenu. (Megas– Protos, Diakonos– doolos/slave)
 • Mtumwa hana cheo, na yeye ni mali ya Bwana wake.

MWISHO

¨ Mamlaka na ukuu huja pamoja na kuwajibika, unyenyekevu na upendo.

¨ Je, unamfuata Kristo katika njia ya sadaka, kujikataa na mateso,

¨ Je, unamfuata Kristo bila masharti Yote?

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *