Swahili Service WANAWAKE SABA WENYE IMANI YA BIBLIA

MARIAMU-IMANI INAYO ABUDU

LUKA 10:39

UTANGULIZI

Mariamu wa Bethania alikuwa dada mkubwa wa Martha na Lazaro. Huyo mariamu aliabudu kwa miguu ya Kristo. Yeye anaitwa Mariamu wa Bethania. Bethania ni Kijiji karibu na mji wa Yerusalemu. Nyumba ilikuwa ya Martha pengine Martha alikuwa mjane. Martha ni yeye alaiyemualika Yesu Kristo kwake (Luka 10:38) pengine Mariamu alikuwa ndiye dada mkubwa kwa maana jina lake lametajwa kanza. Yesu alikaa kwa jamii hii wakati  ametembelea Bethania.

I.   IMANI HUTAFUTA UWEPO WA YESU KRISTO (10:39)

 • Mariamu alimpaka Kristo mafuta ya bei ya juu.
 • Yesu alisema “Mwacheni aiweke” (v.7)
 • Mariamu alifanya chochote kile kuabudu.

II.   IMANI INAMCHANGUA YESU KWANZA.

 1. Martha alichangua karama yake ya kiroho– Yaani ukarimu (Hospitality)
 • Mariamu alichangua kuabudu (Luka 10:46)
 • Mariamu kwanza alichangua kuhudumiwa roho yake kuliko chakula.
 • Kwanza hudumiwa roho yako, ndicho kitu cha maana zaidi.

III.  IMANI INAMSIKILIZA YESU KRISTO (Luka 10:39)

 • Imani humsikiliza Mungu– Mwanadamu hataishi kwa mkate pekee lakini kwa kila neno.
 • Wakati wa kifo chake Lazaro, Kristo aliomba kumwona mariamu kwanza (Yohana 11:28)

IV.   IMANI HULETA MASWALI KWA YESU KRISTO (Yohana 11:32)

 • Mariamu kwanza aliabudu na baadaye maswali.
 • Kwanza muabudu Mungu halafu shida zako fuatisha.

V. IMANI INAABUDU KWA SIFA NA SHUKRANI.

 • Imani huwa na shukrani nyingi (Wafilipi 4:6-7)
 • Shukrani ni msingi wa ibada na maombi.
 • Mafuta ya bei na gharama ya juu.
 • Ibada lazima iwe sadaka.
 • Kwa miguu ya Mwokozi kuinama chini zaidi.

VII. IMANI UPATA DHAWABU             (Luka 10:41-42)

 • Mariamu alichangua jambo lililojema kwa Imani.
 • Mariamu alichangua kisichoweza chukuliwa kutoka kwake. Ibada na huduma kwa nafsi yake.
 • Wakati wa mwisho- “Mwacheni” Mariamu -(Yohana 12:7)
 • Sifa na ibada ni mambawa mbili ya maombi.
 • Katika Agano jipya, sadaka si fungu la kumi, lakini ni kutoa yote kwa Yesu. Mariamu alitoa yote.
 • Tunatoa kulingana na jinsi tulivyo samehewa na Bwana (Luka 7:38-50)

 

MWISHO

 • Je, Umemwanga maisha yako kwa Kristo kwa Imani?
 • Je , ni kitu gani unacho mwangia maisha yako?

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *