Swahili Service WANAWAKE SABA WENYE IMANI YA BIBLIA

MARIAMU MAGDALENE – IMANI INAYOMFUATA KRISTO

SOMO:  LUKA 8:1-3, YOHANA 20:11-18

UTANGULIZI

Mariamu Magdalene ni mfano mzuri wa mwanamke ambaye shetani alikuwa amemuharibu kabisa. Lakini baada ya kuponywa na Yesu Kristo, Mariamu Magdalene alitumiwa na  Mungu Zaidi. Mariamu Magdalene alikuwa mtu wa mwisho msalabani (Marko 15:47)

Mariamu Magdalene ndiye mtu wa kwanza   kaburini mwa Yesu Kristo.(Yohana 20:1). Marimau Magdalene ndiye wa kwanza kuhubiri habari njema ya kufufuka kwa mwokozi (Mathayo 28:8). Mariamu Magdalene alikuwa katika maombi ya kwanza (Matendo 1:14).    Mariamu Magdalene alikuwa chombo cha shetani hapo awali (Pepo saba) (Luka 8:1-2). Mariamu Magdalene aliokoka (Luka 8:3).     Mariamu alimtumikia Kristo (Luka 8:3).       Mariamu alikuwa mhubiri wa injili (Yohana 20:11-18). Maana yake ni Kinara (watch tower). Imani ya kweli inamfuata Kristo-

Hebu tuone:-

I.  WALIOPONYWA WANAWAPONYA WENGINE (Healed people Heal Other people)

 • Imesemwa kwamba watu waliojeruiwa huwajeruhi watu wengine. Lakini kinyume chake pia ni kweli.
 • Tunapo ponywa na Kristo, tunamsaidia kuwaponya wengine.
 • Hawa wanawake Yesu Kristo aliwaponya.
 • Pepo wachavu waondolewa kutoka kwao.
 • Magonjwa sungu yaliponywa na Kristo.
 • Mariamu Magdalene alitolewa pepo saba.
 • Walioponywa na Kristo wanajitoa kwa Bwana naye anawafanya waponyaji.
 • Magdalene alielewa zaidi kuponywa na kukombolewa.
 • Pepo saba– saba ni nambari ya ukamilifu-yaani Magdalene alikuwa chini ya shetani kabisa.
 • Pepo wachafu wanaingia ndani ya mtu kwa sababu ya dhambi (Yohana 8:34-36)
 • Pepo wachafu wanaonekana kila mahali hivi leo. Ulevi, usherati, kupenda vitu, ulafi, ubinafsi, kiburi etc.
 • Shetani alikuja kuiba, kuua na kuharibu (Yoh.10:10) kutumia vibaya, kufanya kitu cha maana kuwa bure. Hali ya kuchota maji na kupasua kuni. Magdalene alikuwa na pepo saba ndani yake– Lakini Kristo.

II.  WALIOPONYWA HAWANA KITU CHA KUFICHA NA KULINDA (Healed people don’t have an image to protect)

 • Magdalene hakuwa na kiburi tena.
 • Kila mtu alimfahamu Magdalene.
 • Wengi wetu tunaficha recordi ya dhambi zetu za kale.

 

 • Magdalene hakuwa na haja tena kujificha mbele ya watu.
 • Tunapojali sana maisha na ushuhuda wetu, hatuwezi kuwasaidia wengine.

III. WALIOPONYWA WANAMTUMIKIA KRISTO NA MALI ZAO.

 • Magdalene pamoja na wanawake wenzake waliingia kwa huduma ya Kristo, walimtumahi Kristo kwa maisha yao yote. Waliwasaidia  wengine kupata uponyaji wao.
 • Kumfuata Yesu Kristo ni pamoja na kutoa mali na wakati wetu kutumika.
 • Imani ya Mariamu Magdalene ilimfanya kumfuata Kristo. Kumfuata Kristo ni kudhamini kazi ya Kristo (Luka 8:3). Mfuasi wa Kristo anaufahamu msalaba na kaburi ya Kristo. (Marko 15:41,40)

 

MWISHO

 • Imani ya Kumfuata Kristo mpaka mwisho ilikuwa dani ya Magdalene.
 • Je, umeamua kumfuata Kristo mpaka mwisho?

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *