Swahili Service

MSAADA KUTOKA JUU

SOMO:  ZABURI 121:1-8

UTANGULIZI

Dunia hii ni mahali pa vita kali. Bila msaada kutoka juu tutashindwa kabisa, tuta shushwa na kupata aibu, pasipo msaada kutoka juu watu watakusahau na kukuacha. Tazama maisha ya Yusufu (Mwanzo 40:9-14). Yusufu alitarajia msaada kutoka kwa mwanadamu, lakini huyu mtu alimsahau Yusufu. Yusufu alikuwa amemwomba mambo mawili;

 1. Nikumbuke , ndugu yangu na kunionea fadhili.
 2. Taja jina langu kwa Farao na kunitoa katika ngereza.

Lakini huyu mkuu wa wanyweshaji hakukumbuka Yusufu, alimsahau.

Ni maombi yangu wewe na mimi tutakumbukwa na Mungu na watu leo.

Baadaye huyu mtu alimkumbuka Yusufu kwa uwezo wa Mungu. Mungu atawalazimisha watu wakukumbuke.

Hebu tuone:-

 

 

I.  MSAADA WA MUNGU UNASHINDA VITA VYA MAISHA (Waamuzi 5:20, Isaya 50:9)

 • Sisera alikuwa hodari sana, msaada kutoka juu ulimwangamiza.
 • Anayepigana nawe anapigana na Mungu mwenyewe.
 • Malaika walitoka Mbinguni na kupigana na Sisera.
 • Malaika wa Mungu watapigana na kuwamaliza adui zako (II Mambo ya Nyakati 26:3-7)
 • Msaada wa Mungu ulifanya kuta za Yeriko kuanguka (Yoshua 5:13-14, 6:20)
 • Si sauti na kelele zao– Mungu ni yeye aliangusha kuta za Yeriko.

II.  NGUVU ZA MUNGU ZINAFANYA KAZI KATIKA KILA ENEO LA MAISHA ( II Mambo ya Nyakati 26:15)

 • Uzia mfalme wa Yuda alisaidiwa mno ajabu hata akapata nguvu.

Þ Nguvu za fedha.

Þ Nguvu za kusoma

Þ Nguvu za Kiroho

 • Msaada wa Mungu unajua jinsi ya kukutafuta ulipo.
 • Nguvu za Mungu zinamfunika mtu wa Imani na kumsaidia ajabu.

 

III. MSAADA WA MUNGU UNAFUNGUA MLANGO WA WASAIDIZI    (I Mambo Ya Nyakati 12:16-18)

 • Msaada wa Mungu unawavuta watu kukusaidia.
 • Kazini unapata msaada,
 • Katika uchumi wako msaada,
 • Katika masamo yako msaada
 • Katika jamii msaada.

IV.  MSAADA WA MUNGU UNAZUIA AJALI NA MIKOSI (Zaburi 121)

 • Msaada wa Mungu unapokujia, Mungu anakuifadhi.
 • Jina lako linawavutia wasaidizi kwako.
 • Neno lako litaalika kibali.
 • Roho yako itaalika kila mtu kukusaidia (I Nyakati 12:21-22)
 • Mungu amekupa ahadi yakukusaidia daima

 

MWISHO

 • Msaada wangu u katika Bwana.
 • Bwana atakulinda na mabaya yote hata milele.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *