Swahili Service

MSAADA WAKO UNATOKA WAPI?

                                                                                          

                SOMO:  ISAYA 31:1-7,

                              ZABURI 121:1-8

UTANGULIZI

Kama watoto wa Mungu tunaitaji kumtegemea Mungu pekee. Lakini si kutafuta msaada kutoka miungu na sanamu hau kwenda katika njia ya Dunia hii. Msaada unaweza kupatikana Misri, Misri ni mahali mbali na mapenzi ya Mungu. Misri ni mfano wa dunia, haijalishi mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini Bwana humuokoa kutoka kwa mateso yote.

Msaada kutoka  kwa Mungu huleta Amani na       furaha, lakini msaada kutoka misri ni laana. Hijalishi mateso yote ya mwenye haki, Mungu anaweza kukomboa (Zaburi 34;19-22)

Msaada wetu hupatikana kwa Bwana, hivyo hakuna sababu ya kwenda Misri, (2 Wafalme 1:2-4). Mfalme Asa alikufa mbele ya wakati wake, maana katika ugonjwa wake hakumwomba Mungu  (II Nyakati 16:12-14)

Hebu Tuone:-

I.   SABABU ZA WATU KUTAFUTA MSAADA KUTOKA MISRI

 1. Kukosa subra na uvumilivu, na kupenda njia ya haraka.
 • Wengi wetu wanaenda duniani kwa kutaka matokeo ya haraka.
 • Mfalme Ahazia alitumana kwa Mungu wa Ekroni kujua atakufa hau ataishi.
 1. Ujinga wa kutojua usaidizi unaopatikana kutoka kwa Mungu.

 

 • Wengine katika kanisa hawajaokoka kamilifu hau uhusiano wao na Mungu si kamilifu.
 • Wengine hawaelewi shida za Kuomba msaada kutoka kwa watu wa dunia hii.
 1. Wengine hawako tayari kulipa gharama ya kukaa katika utakatifu na kupata msaada wa Mungu.
 • Wengine hawako tayari kuishi maisha ya kujitenga na dhambi.
 1. Wengine hawako tayari kuacha tamaa na anasa za misri
 • Wana wa Israeli walipenda kurudi Misri kwa maana ya kitunguu na mboga za misri.
 1. Wengine wamekubali uogo wa shetani, wanatengemea manabii wa uongo wawaeleze kile wanataka kusikia.
 2. Wengine wanaendelea na kushikana na walimwengu kupokea ushauri (Zaburi 1:1-3)
 3. Hofu inaoleta fadhaa na kutoamini Mungu.

II.   UKWELI WA KUPOKEA MSAADA KUTOKA MISRI.

 • Misri ni dunia hii hivyo wengi wanaingia katika agano na nabii wa shetani. Agano na shetani inampa shetani haki katika maisha.
 • Kuwaendea manabii wa uongo kupokea maombi kwao na unabii.
 • Kukula kiapo mbele ya sanamu, kuendeleza ndoa, biashara na mali.
 • Kuwaendea waganga kusomewa nyota na utabiri wa maisha ya mbele.
 • Kutoa sadaka hili kupokea kibali na kujikinga na maovu.

III. JINSI YA KUPOKEA UKOMBOZI     KUTOKA MAMBO YA MISRI.

 • Ukombozi unapatikana katika jina la Kristo.
 • Yesu kristo alikuja duniani ili azivunje kazi ya ibilisi (I Yohana 3:8)

 

 • Kupokea ukombozi dhidi ya kazi za ibilisi ni lazima:
 1. Kuokoka– Ukombozi hufuata wakovu.
 2. Vunja kila Agano yako na ibilisi na watu wa giza.
 3. Kataa kabisa kila agano ya shetani. Omba damu ya yesu Kristo juu ya maisha yako.
 4. Toa kabisa vitu vyote vya shetani vilivyo katika mwili, nguo na nyumbani . Hii ni pamoja na vitu vyote ulionavyo kwa kupokea nguvu na uwezo, kinga na bahati njema.
 5. Omba Mungu wa Mbinguni kupokea ukombozi na utakatifu.
 6. Uwe na uhusiano wa karibu na Mungu.
 7. Omba Mungu kudumisha ukombozi wako kwa kukaa juu zaidi ya dhambi

 

MWISHO

 • Je, msaada wako unatoka wapi ?

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *