Swahili Service UKOMBOZI

MUACHANO MBAYA (EVIL DIVERSIONS)

YONA 1:1-17

UTANGULIZI

Muachano ni kuacha njia iliyo sahii. Muachano ni kubadilisha muelekeo. Muachano ni kila jambo linalo chukua mafikira yako kutoka kwa shabaha yako. Muachano unaweza kuwa mbaya hau mzuri. Maisha kama jinsi safari, safari inao mwanzo, muelekeo na mwisho. Mungu anao mpango wa Ajabu kwa maisha ya kila mmoja wetu. Maisha ya mtu inaweza kugeuzwa na shetani katika muachano wa kishetani. Yona 1:1-17, Yona alibadilisha muelekeo wa safari yake. Muachano wa safari yake ulileta maovu kwa watu wengi sana. Wafanya biashara walitupa mali yao baharini kwa sababu mtu mmoja aliyekuwa katika muachano mbaya alikuwa katika chombo. Yona alilala wakati dhoruba iliwaamusha wengine wote. (7-17). Je, ni roho gani inayomfanya mtu kubandilisha muelekeo na kwenda katika muachano mbaya ? Roho gani ilimfanya Yona kubandilisha safari ya kwenda Ninawi? Hata mtu akiwa nabii wa Mungu anaweza kuingia katika muachano mbaya.

Hebu tujifunze:-

I.  DALILI YA MUACHANO MBAYA

 • Muachano mbaya unafanyika katika giza.
 • Muachano mbaya unafanyika wakati shetani amefaulu kukuweka katika giza.
 • Jinsi mtu amekaa katika giza ndivyo muachano mbaya ulivyo mkali zaidi.
 • Watu waovu wanaweza kuona maisha ya mtoto anapozaliwa, ndiposa wakampa muachano (diversion) katika maisha yake.
 • Uenda, kabla ujaokoka maisha yako yalipewa muachano tayari. Hivyo safari ya maisha yako yalibandilishwa.

II. HAINA YA MUACHANO ( CLASSES OF EVIL DIVERSION)

 1. Muachano mbaya unao julikana (Conscious)
 2. Muachano mbaya husiojulikana (Unconscious)
 3. Muachano mbaya wa urithi (Inherited)
 4. Muachano mbaya wa kupewa (Transferred)
 5. Muachano mbaya wa kupenda (personal decision)

Ni maombi yangu kwamba safari zako zilizo ovu, Bwana atazivunja leo katika jina la Kristo Yesu.

 • Kama mtu alizaliwa awe mwalimu hau fundi, lakini wazazi wakamfanya awe daktari wa dawa, huyu daktari ataumiza wagojwa.
 • “Samaki hawezi kubarikiwa inje ya maji”
 • Shetani anatuletea muachano mbaya ili tusifanye mapenzi ya Mungu, na mtu hasifikie hatima yake.

III. LENGO YA MUACHANO MBAYA

 1. Kuweka mtu mbali na Mungu.
 2. Kukatisha hatima ya mtu.
 3. Kufanya shetani kutawala maisha ya mtu.
 4. Kufanga watu ili wasiweze kuokoka na kukutana na Mkombozi wao.
 • Mhubiri anaweza kupewa muachano mbaya ili watu wasiokoke.
 1. Kuaribu maisha ya watu, kuwatoa watu kwa Baraka, baadaye watu waingie motoni.

IV.  MAISHA YALIO TUMIKA MBAYA NI NINI?

 • Maisha bila sababu, lengo na shabaha.
 • Maisha yalio pata muachano mbaya.
 • Maisha bila maana, maisha ya kuchanganyikiwa.
 • Mke hau mume anaweza kukuletea muachano mbaya.
 • Marafiki wanaweza kukuletea muachano mbaya.

V.  NI NANI AGENTI WA MUACHANO MBAYA?

 1. Agenti wa kwanza ni roho zidanganyazo (seducing Spirits) (I Tim. 4:1)
 • Roho za udanganyifu ni nyingi leo, kwa maana hizi ni siku za mwisho.
 • Roho hizi lengo lake ni kushika watu wa Mungu mateka na kuwaweka katika muachano.
 • Roho hizi zinafanya kazi kupitia udhaifu wa mtu, (hasira, tamaa mbaya, kiburi)
 1. Agenti wa pili ni roho fanana (familiar spirits)

VI.  JINSI YA KUPATA USHINDI DHIDI YA MUACHANO MBAYA.

 • Pima kila roho
 • Fahamu Neno la Mungu
 • Uwe hodari katika maombi.
 • Usiwe mjinga kiroho
 • Funga mwenye nguvu-undanganyifu (seduction)
 • Funga kila njia za udanganyifu dani ya maisha yako.

MWISHO

Omba:

 1. Nina Kemea Roho ya Muachano mbaya , katika Jina La Yesu Kristo.
 2. Ninakemea Kila roho ya udanganyifu– Katika Jina la Yesu Kristo.
 3. Ninatubu kila muachano mbaya ndani yangu katika Jina La Yesu Kristo.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *