Swahili Service

MUNGU ANAPO PIGANA VITA VYAKO

KUTOKA 14:14

UTANGULIZI

Ni vizuri sana kumruhusu Bwana kupigana vita vyako kwa maana Mungu anapokupigania ushindi ni lazima. Leo tuna tazama njia nane Mungu atakupigania vita. Kila mwana wa Mungu yuko katika vita vya kiroho na kimwili pia. Biblia inatufundisha kwamba Mungu wetu Yehovah ni mtu wa vita. Ona Isaya 63:4, Warumi 12:19. Hivi omba maombi yafuatayo “ Ee, Bwana, nipiganie vita katika Jina La Yesu Kristo”, “Bwana anipigania vita name nitanyamaza kimya” (Kutoka 14:14)

Hebu tuone njia nane za vita za mungu kwa niaba yetu:-

 1. BWANA ANAFADHAISHA ADUI ZAKO (Kutoka 14:24-26)
 • Mungu alipoona kwamba jeshi la Misri lilikuwa karibu sana na wana wa Israeli, Mungu akayaondoa magurudumu ya magari yao.
 • Magari ya Misri yakaenda kwa uzito.
 • Hata wamisri wenyewe walifahamu Mungu anawapigania Waisraeli!
 • Baadaye Farao na Jeshi lake walizama maji katika bahari ya Shamu.(Kutoka 14:27-28)
 • OMBA- “Ee Bwana zamisha adui wanaonikimbiza katika Jina La Yesu kristo.”
 1. BWANA ATATUMA MALAIKA WAKE MBELE KUPIGANA NA ADUI YAKO (II Samweli 5:23-25)
 • Hapa Malaika wa Bwana ndiye alipigana vita.
 • Daudi na Jeshi lake walifanya kumalizia vita.
 • OMBA- “Ee Bwana tuma malaika wako mbele yangu kupigana vita vyangu– Katika Jina La Yesu Kristo.”
 1. BWANA ATAFANYA ADUI ZAKO KUSIKIA SAUTI ZA AJABU (II Wafalme 7:5-7)
 • Sauti za magari zaliwafadhaisha washami mpaka wakatoroka wakaenda zao.
 • Washami waliacha kila kitu.
 • OMBA- “Ee Bwana fanya adui zako kusikia sauti za ajabu na kuniacha kwa Amani.”
 1. BWANA ATATUMA MALAIKA KUWAUA ADUI ZANGU (II Mambo ya Nyakati 32:21)
 • Mfalme wa Shamu alimtumia mfalme Hezekia barua ya kutisha sana.
 • Bwana alimjulisha mfalme Hezekia kwamba malaika atashughulikia jambo hilo.
 • Asubuhi yake jeshi la shamu lilikuwa mauti.
 • Mfalme wa shamu aliuliwa na mwanaye.
 1. BWANA ATAWAFANYA ADUI ZAKO KUOTA NDOTO MBAYA (Waamuzi 7:9-10, 13-14)
 2. Bwana atawapiga mawe adui zako, mawe kutoka mbinguni (Yoshua 10:10-11)
 3. Bwana atatumia mambo ya asili kuwaangamiza adui zako (I Wafalme 20:29-30)
 • Ukuta uliwaangukia watu 27,000, wote wakafa.
 1. Bwana atawafanya adui zako kumalizana wao kwa wao. (II Mambo ya Nyakati 20:17, 22-25)
 • Mungu aliwafanya adui kupigana wao kwa wao.
 • Tena Mungu aliwafanya kwenda vitani na fedha zao, dhahabu na mali yao ya dhamani kuu.
 • Bwana atawafanya Adui zako kukupa utajiri wao.

 

MWISHO

 • Kwa nini tumwobe Mungu kutupigania vita;
 1. kuna vita nyingi sisi wenyewe hatuwezi.
 2. Vita nyingi vya kiroho vinashidwa kwa nguvu za Bwana pekee.
 3. Bwana anapotupigania vita, mwenyewe anapokea sifa na utukufu.
 4. Bwana anapokupigania vita, shetani hatacheza na wewe tena.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *