MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANI Swahili Service

MUSA:MTU WA IMANI: WAEBRANIA 11:23-29

UTANGULIZI

Kwa Wayahudi Musa ndiye mtu mwenye heshima kuliko wote katika historia yao. (Kumbu Kumbu 34:10-12). Kwa Israeli wote Musa ndiye Nabii mkuu, mwanasheria mkuu na mwana historia. Aliandika vitabu tano vya kwanza vya Biblia. Musa ndiye mtakatifu zaidi ya wote. (Hesabu 12:3). Musa aliwakomboa wana wa Israeli kutoka utumwa wa miaka 400 Misri. Musa aliishi kwa Imani. Njia ya Mungu ni njia ya Imani.

Hebu tuone:-

I. KWANZA, MUSA ALIKUWA NA URITHI WA IMANI. (Waeb. 11:23-24)

 • Imani ya Musa alianza na wazazi wake.
 • Wazazi wake waliona Musa ni mtoto mzuri yaani special.
 • Wazazi waliona kwamba mtoto Musa hakuwa mtoto kawaida.
 • Kila mzazi anaona mtoto wake ndiye mrembo zaidi, hata ingawa uso wake unaweza kupendwa na mama yake pekee.
 • Amri ya Farao ilikuwa watoto wauliwe, idadi ya wana Israeli ilikuwa juu zaidi.
 • Amramu na Yokebedi wazazi wake Musa walikuwa wa Imani, wakamficha mtoto Musa kwa miezi ya kwanza mitatu.(Kutoka 6:20)
 • Imani haingopi hatari. Imani hufukuza hofu.
 • Baada ya miezi mitatu, Musa alichukuliwa na Binti Farao, Imani huachilia jambo mikononi mwa Mungu.

II. PILI, MUSA ALIKUWA NA IMANI YA KUCHAGUA (11:24-26)

 • Musa Alikataa– kuitwa mwana wa binti Farao. (v.24)
 • Musa Alichangua– Afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha (v.25)
 • Musa Alihesabu– Kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri. Alitazamia malipo.
 • Musa aliweka mambo yote katika mizani
 • Musa alikuwa amesoma elimu yote Misri. (Matendo 7:22)
 • Chuo alichosomea Musa kiliitwa “The Temple of the sun” University. Chuo hiki kilikuwa “Oxford ya dunia ya kale”
 • Musa alisoma, science, historia, Geographia, Dawa, nyota, kemia, philosophia, uchoraji, uimbaji na masomo yote ya jamii.
 • Musa alisoma masomo ya vita, alikuwa miaka 30 alikuwa tayari jemedari wa vita. Alishida vita ya Misri na Ethiopia.
 • Lakini Musa alichangua Yesu Kristo na wokovu kamili.
 • Musa aliona dhambi na fahari zake ni kwa kitambo tu.
 • Musa aliona afadhali utajiri wa Mungu, kuliko anasa.

III. TATU. MUSA ALISTAHIMILI WAKATI  HASIPOONA KWA MACHO

 • Musa aliacha Misri, alitoka kabisa
 • Petro, Yakobo na Yohana waliacha nyavu zao zote (Luka 5:11)

IV. NNE, MUSA ALIMTENGEMEA MUNGU WAKATI ASIPO ELEWA (11:28)

 • Musa alipotoka Misri baada ya ukombozi aliendelea Pasaka na kunyunyiza damu.
 • Musa aliishi chini ya damu ya Mwana Kondoo

V. TANO, MUSA ALIKUWA NA IMANI YA KISIMAMA KATIKA BAHARI MUNGU AFANYE KAZI YAKE. (11:29, Kutoka 14)

 • Musa aliwaambia Israeli “Simameni Imara” muone wokovu wa Mungu. (Kutoka 14:13-16)
 • Kwa Imani Mungu aliwapigania Israeli (Kutoka 14:21-22)

 

 

MWISHO

¨ Imani ya kweli  husimana imara katika dhoruba

¨ Imani ya kweli, hukataa, huchangua huhesabu

¨ Je, Imani yako imetenda nini?

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *