Swahili Service

MWALIKO WA KUJITOA

MWANZO 7:1-16

UTANGULIZI

Biblia ni kitabu cha mialiko !Kutoka Mwanzo saba mpaka mwisho wa Ufunuo Mungu yupo katika kazi ya kualika. Hivyo natumfuate Mungu katika mialiko yake kwetu. Leo tunatazama mwaliko wa kwanza kutoka kwa Mungu. Neno njoo imetumika mara 1,972. Mwanzo 7:1 ndiyo ya kwanza. Mungu alimwalika Nuhu na Jamii yake kuingia ndani ya safina. Nuhu na jamii yake walihitaji kupokea na kujitoa kuingia katika ile safina. Bwana anapotuita tunahitaji kujitoa .

Hebu tuone:-

I.  IFADHI YA MWALIKO HUU. (Mwanzo 7:1)

 • Safina ilikuwa katika Mesopotamia ya zamani. Urefu wake 450ft, 75ft upana na 45ft kina chake.
 • Safina hii ilijengwa na mhubiri Nuhu na wanawe; Shemu, Hamu na Japheth. Safina ilikuwa ifadhi yao.
 • Kwa miaka 120, jamii ya Nuhu kwa imani walifanya kazi ya kujenga safina.
 • Safina hii ilikuwa maficho ya Mungu kwa jamii ya Nuhu.
 • Mwanzo 6:1-4; Kulikuwa ndoa katika watoto wa Mungu na watoto wa shetani, watoto wa Sethi ma watoto wa Kaini.

 

 

 • Mwanzo 6:5; Mungu aliona dhambi za wanadamu, mawazo yake yalikuwa maovu siku zote.
 • Mwanzo 6:11-12; Mungu aliona dunia ilikuwa imeharibika, dhuluma ilijaa dunia.
 • Mwanzo 6:6-7: Suluhisho ya Mungu ilikuwa kuaribu watu wote.
 • Lakini Mungu aliwajengea safina kuwa ifadhi na maficho (sanctuary) kwa wakovu wao.
 • Leo hii Kristo ndiye safina ya salama kutoka kwa dhoruba inayokuja duniani.
 • Kristo pekee ndiye maficho na wakovu wa dunia hii. Mwaliko wa kuingia umetangazwa. Je, utaingia dani ya safina (Yoh.14:6, Matendo.4:12, Matendo 16:31).

II. MWALIKO ULITOKA KWA MUNGU MWENYEWE (7:1)

 • Mwaliko wa kuingia haukutoka kwa Nuhu lakini kwa Mungu. (Mwanzo 6:8) “ Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana”
 • Kama si neema ya Bwana, Nuhu angaliweza kujua juu ya gharika
 • Ikiwa umeokoka, ni kwa neema ya Bwana.
 • Mtu hawezi kumjia Mungu kama si kwa neema ya Bwana (Waefeso 2:1-10)
 • Hatuwezi kujua juu ya gharika bila Bwana.
 • Hatuwezi kujua ya Msalaba, na juu ya dhambi bila neema ya Mungu.

III. USALAMA WA MWALIKO HUU. (7:16)

 • Mungu aliwafungia ndani ya ile safina wakawa salama.
 1. Mungu hakuwaambia “Enendeni kwa safina” Lakini “Njooni katika safina “. Mungu tayari alikuwa katika safina.
 2. Mungu aliwafungia ndani. (Waefeso 4:30)
 3. Nuhu alikuwa salama katika safina kwa nguvu za Mungu (I Petro 1:5)
 4. Maji yalipopanda juu zaidi, safina ilielea juu zaidi (Mwanzo &:19-20, Warumi 5:20)

 

MWISHO

¨ Nuhu aliokoka gharika kwa sababu ya imani.

¨ Safina ilikuwa moja tu- Njia ya kuokoka ni Yesu pekee

¨ Je, Mungu anakuita uokoke ? Mlango ni wazi.

¨ Je, umeokoka ? Basi, Amini kwamba wewe ni salama ndani ya Kristo.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *