MIALIKO MIKUU KATIKA BIBLIA Swahili Service

MWALIKO WA UTAKASO

ISAYA 1:18

UTANGULIZI

Nabii Isaya alitumika katika wakati kama  wakati tulionao hapa kwetu Kenya. Inchi ya Israeli ilikuwa imemwacha Mungu na njia zake. Watu wa Mungu walikuwa wanaishi katika dhambi na ibada za sanamu.

(v.2) watu walikuwa wamemuasi Mungu.

V.3: Israeli walikuwa wamemkataa Mungu, kwa kweli walikuwa wameshidwa akili na wanyama.

V.4: Walichukua mzigo wa dhambi na uovu.

V.5: Walikuwa wagonjwa wa moyo na kuzimia

V.7-8: Ubaya ulienea kila mahali.

V.9-10: Walikuwa kama Sodoma na Gomora.

V.11-15: Ibada zao zilikuwa chukizo kwa Mungu.

V.9: Mabaki wachache ndio walibaki Israeli yote.

Watu hawawezi kumtafuta Mungu kwa nguvu zao wenyewe. (I Yohana 4:19, Waefeso 2:1-3, Luka 19:10).

Bwana anawaalika watu wa Israeli wamnjie. Hivi leo, Mungu anawaalika, wenye dhambi, wamjie wapate utakaso.

Hebu tuone:-

 

I.  TATIZO YA MWALIKO HUU.

 1. Haya, njoni tusemezane asema Bwana.
 • Mwaliko huu ni Amri kutoka kwa Mungu.
 • Mungu anafahamu mioyo yetu, anajua dhambi zetu.
 • Neema na Rehema zake zipo kwa wote wamnjiao.
 1. Mungu anafahamu dhambi zetu, anajua kwamba sisi tu wenye dhambi, waovu na wenye kupungukiwa sana. (Ufunuo 22:17, Yohana 7:37, Mathayo 11:28)
 2. Mungu anafahamu hali ya mioyo yetu kuliko sisi wenyewe. (Warumi 5:6-8)

II.  HARAKA ZA MWALIKO HUU.

 1. Amri ya Mungu ni tumjie sasa, bila kuchelewa.
 • Mungu anaona njia zetu na muelekeo wa mioyo yetu.
 1. Hivyo ndivyo ilivyo kwa wote wasio haki mbele zake. (II Wathesa.1:8-9, Zaburi 9:17, Mathayo 13:42, Ufunuo 14:11)
 2. Kama umeokoka, kwenda mbali na Mungu kunaleta nidhamu zake (Waeb.12:6-11)
 3. Mungu anajua jinsi mambo yatakuwa mbaya zaidi kwa wemye dhambi. (Mwanzo 6:3, Mithali 27:1, II Wakor.6:2)

III. URAFIKI WA MWALIKO HUU.

 1. “Haya, njoni tusemezane, Asema Bwana.”
 • Bwana anasema tusawazishe mambo ya mioyo yetu – Tusemezane.
 1. Mungu anawaita watu binafsi, wala si kwa jumla. (Yohana 16:7-13)
 2. Je, umesikia mwaliko huu wa Mungu kibinafsi?

 

IV.  AJABU YA MWALIKO HUU.

 1. Ahadi za Mungu kwa Israeli, ikiwa watamjia ni kwamba dhambi zao zijapokuwa nyekundu sana, zitakua nyeupe kama theluji.
 2. Mwaliko huu ungalipo leo. (Isaya 64:6)
 3. Je, wewe una hakika dhambi zako zime samehewa?

 

MWISHO

¨ Bwana anakuita leo, sikia mwito na mwaliko wake.

¨ Bwana anakuita nje ya korti kusemezana leo.

¨ Wamebarikiwa wanao tii sauti ya Bwana anapowaita.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *