IBRAHIMU: KUMFUATA BWANA KATIKA IMANI Swahili Service

MWITO WA MAISHA YA IMANI

Ni watu wachachetu  tu nje ya Yesu Kristo wamechangia katika historia ya ulimwengu kama Ibrahimu.Ibrahimu anaheshimika na zaidi ya nusu ya watu wa dunia. Wayaudi,Waislamu na Wakristo wanamheshimu Ibrahimu kiasi cha kumwabudu.

Hivyo dini za Uyaudi,Uislamu na Ukristo zinaitwa dini za Ibrahimu. Ibrahimu ni mfano mwema wa wale wanaoishi kwa imani (Waebrania 11:8-19, Yakobo 2:23) Ibrahimu anaitwa ‘Rafiki wa Mungu’.

Leo tunatazama jinsi mungu alivyomwita na kumpa ahadi ya kumbariki .Ibrahimu aliishi zaidi ya miaka 4100 iliyopita lakini sifa zake na maisha yake ya imani ndio kiini cha imani ya kuokoa . Hebu tujifunze;

 1. MAISHA DUNI YA IBRAHIMU -MIAKA YA DHAMBI (THE WRETCHED YEARS) 11:26-30
 • Miaka ya dhambi, Ibrahimu hakujulikana na watu
 • Miaka hiyoIbrahimu alikuwa hana jina katika bahari ya idadiya wanadamu.

A.Mahali pa Nyumba Kale ya Ibrahimu

 • Uru wa wakaldayo,palikuwa katikanchi ya leo –Iraq
 • Uru ulikuwa mji mkuu katika biashara.Wakaldayo, Wahindi na Waafrika walikutana Uru kwa biashara zao
 • Uru ulikuwa mji wa elimu, maktaba kuu ilijengwa hapo Uru.
 • Watu wa Uru walikuwa wakulima na wafugaji wa ng’ombe na kondoo.

B.Shida ya nyumba kale ya Ibrahimu

 • Watu wa URU ya wakaldayo walikuwa watu wa ibaada za sanamu
 • Waliabudu mungu wa jua,mwezi na nyota.
 • Uru ulikuwa mji wa uchawi na ibaada ya mapepo (Yoshua 24:2, Mwanzo 31:30-34, Isa 51:1)
 • Mungu LImuita Ibrahimu kutoka katika dhambi ya watu wa Uru

     C. Machungu ya Nyumba ya kale ya Ibrahimu

 • Uru palikuwa pahali pa uchungu,mauti na hofu (v. 28-30)
 • Sisi nasi tulikuwa hivyo;dhambi, hofu na mauti.(waefeso 2:1-3)
 1. MAISHA YA UTII NUSU (THE WASTED YEARS) (11:31-32, 12:1)

     A.Mwito wa kutoka (12:1)

     B.Ibrahimu alikosa kutii kwa ukamilifu

 • Alichukuana na Lutu na kubebana na baba yake Tera
 • Tera maana yake ni mahali pa stesheni, mahali pa kuchelewa (a station of delay?)
 • Tera maana yake, kusimama,kupumzika au roadblock
 • Tera alikuwa kikwazo katika safari ya kwenda nchi ya ahadi

     C. Gharama ya kuchelewa (11:32)

 • Miaka ilipita.Kila mwaka unaopita unavuta karibu na karibu
 • Tera alibebana na sanamu zake na miungu ya Uru
 • Miaka yake Ibrahimu iliisha bure(warumi 13:11-14, waefeso 5:16)
 • Kuchelewa ni gharama zaidi, pia hatari sana.

    3 . MAISHA YA FURZA KUU (THE WONDER YEARS) 12:1-3

Baada ya miaka ya dhambi na miaka ya kupoteza katika kuchelewa, mungu alimpa IBrahimu     miaka ya Baraka. Miaka yake ilikuwa 75

   A.Miaka ya Uwepo wa mungu. 12:1 (Waeb 13:5, Zab 37:19)

   B. Miaka ya kumtazama Mungu na utoshelevu wake 12:1-3

 • Nyumba mpya ,uzao,baraka tele,jina kuu,ushindi juu ya adui,kuwa Baraka kwa wengine

   C. Miaka ya Kufahamu mpango na kusudi Kwa Mungu

MWISHO

 • Safari ya maili 1000 inaanza kwa hatua moja
 • Je,umeanza safari yako ya imani?
 • Je, umeokoka,umekata uhusiano wako na watu wa dunia?

 

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *