MITUME WA YESU KRISTO Swahili Service

NEEMA YA MUNGU-MATHAYO

 

SOMO:  LUKA 5:27-32

UTANGULIZI

Kisa cha Lawi, aliyeitwa kwa jina lingine Mathayo ni cha mtu aliyefanya mapatano na serikali ya Roma kutoza ushuru kutoka kwa Wayahudi wenzake. Kazi yake Lawi ilimtenga na watu na jamii yake. Hivyo marafiki zake walikuwa watu wakutoza ushuru. Lawi alitengwa na kuchukiwa na watu, majirani na jamii.

Mabadiliko katika maisha ya Lawi yalianza wakati alipokutana na Kristo. Baadaye, Lawi akawa mtume. Alipookoka Lawi aliwaita marafiki wake kwa chakula na kualika Kristo nyumbani kwake. Jambo hilo halikuwapendeza mafarisayo na waandishi wa sharia na torati. Hivyo wakuu wa dini wakamuliza Kristo “kwanini mnakula na kunywa na wenye dhambi na watoza ushuru?” Je, Maisha ya kale, yatamtenga mtu maisha ya usoni?

Hebu Tujifunze:-

 1. KUJA KWA YESU KRISTO KUNAFANYA WOKOVU KARIBU (Luka 5:27-28)
 • Kristo alijitokeza kumtafuta Lawi mtoza ushsuru.
 • Baada ya kumwita Simoni, Yakobo na Yohana (Luke 5:10)
 • Yesus Kristo alimwita Lawi “NIFUATE”
 • Lawi alichukiwa zaidi , mtoza ushuru alichukiwa kama mbwa, mwenye ukoma na mwenye kulaaniwa.
 • Lakini Yesu Kristo alimwona Lawi, ameketi forodhani.
 • Lawi aliishi maisha ya upweke, aliketi pekee na kuishi pekee.
 • Hivyo Mathayo, Lawi alipotembelewa na Kristo, alipata nafasi ya kuanza maisha yake upya !!
 • Mathayo, Lawi alifanya mabo matatu, Aliacha yote, Akaondoka, Akamfuata Kristo,
 • Lawi aliyaacha yote, maisha ya kale yalikuwa nyuma yake kabisa na milele.
 • Lawi alifanya kama Jinsi John Newton aliye andika wimbo “Katika Neema ya Yesu”
 • John Newton alikuwa muuza watumwa kutoka Afrika kwa inchi za mbali.
 • Katika mwaka wa 1748, Newton alikutana na Yesu Kristo.
 • Newton alikuwa mtumwa wa dhambi na shetani.
 • Katika jiwe la kaburi yake wameandika “John Newton Clerk, aliyekuwa mwenye dhambi, na mwenye biashara ya kuuza watumwa kutoka Afrika, kwa neema ya Mwokozi na Bwana Yesu Kristo, aliokoka, Akasamehewa na kuitwa kuhubiri Imani na Injili aliyejaribu sana kuangamiza”.
 1. WAFUASI WA YESU KRISTO WANAFANYA MABANDILIKO KUPATIKANA HARAKA (Luka 5:28-29)
 • Lawi alionyesha mabandiliko katika maisha yake.
 • Pamoja na kumfuata Yesu Kristo ni lazima kuonyesha mabandiliko.
 • Maisha ya kale na marafiki wa kitambo lazima kuacha.
 • Tunapookoka lazima kuacha ya kale, kuchoma vyombo vya kazi ya giza na kutoka kabisa.
 • Lawi aliwaita marafiki wa kitambo, wakutane na Kristo pia awatangazie kwamba yeye ni kiumbe kipya !!
 • Nyumba ya Lawi ilikuwa center ya injili (Matt.9:10, Marko 2:15)
 • Usiogope, kuachwa na marafiki, biashara na kupoteza kwa ajili ya Kristo Yesu.
 • Yesu Kristo aliacha yote, akawa maskini, hili na sisi tuwe tajiri.

III. PONGEZI YA YESU KRISTO INAFANYA MATUSI YA WENGINE KUWA SI KITU. (Luka 5:30-32)

 • Yesu Kristo aliuliza maswali tatu:
 1. Ni nani anayehitaji tabibu ?- Aliye hawezi
 2. Yesu alikuja kuwaita akina nani?- Wenye dhambi
 3. Kitu gani kinacho hitajika ?- Wenye dhambi wapate kutubu.
 • Yesu Kristo hatafuti walio na jibu, lakini walio na majibu,
 • Yesu Kristo alimpongeza Lawi Mathayo
 • Yesu Kristo hakuwakemea watoza ushuru, bali aliwapongeza kwa kuja kwao.
 • Yesu anwakubali wenye dhambi, lakini aliwakemea mafarisayo na wakuu wa dini.

 

MWISHO

¨ Kila mtakatifu ana historia ya maisha ya kale na kila mwenye dhambi ana maisha ya usoni.

¨ Yesu Kristo alikuja kutafuta wenye dhambi kuokoka. (2 Wakorintho 5:21)

¨ Je, wewe ni chombo cha kuwaleta watu kwa Kristo Yesu.

¨ Nena Jina la Kristo, shiriki upendo wa Kristo, watafute waliopotea dhambini.

¨ Rekembihsa nyumba yako, weka watu wale wangeni mbele ya nafsi yako, Tumika kwa ajili ya Yesu Kristo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *