Swahili Service UKOMBOZI

ROHO YA UTORO

MWANZO 4:12,  KUMBUKUMBU 21:18-21, ZABURI 109:10

UTANGULIZI

Roho ya utoro, hau upako wa utoro na kutangatanga inachangia pakubwa kukosa muelekeo na  kukosa shabaha katika maisha ya watu wengi. Shetani mwenyewe ni mtoro na kazi yake ni kusambaza roho na upako wa utoro na kutangatanga. Katika Mwanzo 4:12, tunaona mtoro wa kwanza duniani “Utakapolima arthi haitakupa mazao yake, utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani”. Katika Kumbukumbu 21:18-21, -watoto wanaweza kuwa watoro, katika Zaburi 109:10-laana ya utoro na kutangatanga na kukopa na kuomba omba. Katika Matendo 19:13-16– Wayahundi wenye kutangatanga (watoro) na wenye kupunga pepo (Exorcists). Katika Ayubu 1:6-7– shetani ndiye mtoro mkuu (Petro 5:8). Katika Luka 15:11-15– Mwana mpotevu alishika roho ya utoro na kutangatanga.

Hebu Tuone:-

I.   ISHARA ZA MTORO (Luka 15:11-15)

 1. Mtoro ni mtu wa shida nyingi na kilio (Sorrowful)
 • Dhambi kila wakati uleta kilio.
 1. Roho ya utoro kila mara ushusha mtu cheo na heshima-Mwana mpotevu alishushwa kutoka kwa ufalme mpaka kulisha nguruwe.
 • Waisraeli hawafungi nguruwe hivyo hii ni kazi ya chini kwao
 • Kazi hii umfanya najisi na aibu kuu.
 1. Mwenye dhambi kila wakati ni mtu aliye mbali na nyumbani. (Zaburi 109:10)
 2. Mtoro ni mtu mwenye ubinafsi sana

II.   MAANA YAKE UPAKO

 • Upako ni jambo la kiroho. Upako ni jambo la nguvu maana ukiwa na upako hamna kuchoka. Mungu hana upako kinyume– kazi yake ni takatifu.
 • Siku hizi ni za mwisho na maovu yamezidi (Luka 21:29-33)

III. ROHO NA UPAKO WA UTORO

 1. Maisha ya mtoro ni maisha yasio laini, ni maisha ya kutangatanga. Maisha ya kutembea bila sababu, kukosa shabaha. Mungu aliziumba vitu vyote siku sita. Siku ya saba alistarehe. Hivyo watu wa Mungu ni watu wa kustarehe nafsi zao.
 • Watoro na roho ya utoro hawana kustarehe.
 • Watoro ni watu wa kutangatanga mji kwenda mji , mke kwenda mke, Mme kwenda Mme, kazi kwenda kazi, nyumba kwenda nyumba, ndoa kwenda ndoa– wana sumbuka hawawezi kukaa.
 1. Watoro wanasumbuliwa na roho ya umaskini.
 • Mtu anapokuwa na roho ya utoro na ufukara, hawezi kuwa tajiri,sababu anayo roho ya kuaribu vitu na mali. (Poor people are also wasteful). Hivyo anasumbuliwa na roho ya kuchanganyikiwa, utumwa kifedha, depression, upweke, kukata tamaa, mawazo ya kijiua na kilio (Sorrows) kuomboleza.
 1. Roho ya utoro inamfanya mtu kutumia fedha zake na mali, mkono wake ushikapo kitu, kinaharibika.
 • Mtu mtoro anaweza kuwa amesoma sana (B.A,BSC,M.A,PhD) lakini roho ya utoro na ufukara inamshika kabisa. Kila aendako anakuwa sehemu mbaya.
 1. Roho ya utoro na upako unafanya mtu kuvua samaki hasipate chochote katika bahari ya maisha. Anaweza kwenda popote duniani hasifaulu kwa chochote. Hivyo ndivyo daktari wa dawa anaosha vyoo, hau PhD anafanya kazi ya kulea mtoto huko nga’ambo.
 2. Roho ya utoro inaleta Baraka zizizo dumu na kupenya bure. (Slippery blessings and unstable breakthroughs and confusion). Mwaka huu uko karibu kwisha, Je, umefika katika malengo yako ?
 • Ikiwa unaposoma Biblia, hau kuomba akili yako inaruka ruka– roho ya utoro himo.
 1. Roho ya utoro ni roho ya kualikwa na roho zingine.
 • Roho ya kutovumilia inavuta roho na upako wa utoro na ufukara. Hawawezi kungoja (Isaya 40:28-31)
 • Watu hawa hawawezi kusubiri na kustarehe, kila wakati wanafanya jambo, kusikiliza ujumbe ni shinda.
 • Watu hawa wanaenda kichaa kwa haraka sana.
 • Wengine wanasema Mungu aliwaambia wawe katika mwendo !!
 1. Roho ya utoro– inafanya mtu kutembea mke hadi mwingine-wengine wanaoa kupitia internet na magazeti, wanapeana shinda zao kwa dunia.
 • Wanaota ndoto za kupanda milima hau gazi mbila kufika mwisho wake !!
 • Kukopesha watu mbila kulipwa, kupeana msahada kwa watu lakini wao wanateseka.
 • Kuingia biashara za kila haina bila utafiti kamili.
 • Kuingia michezo ya bahati na sibu na kamali.
 • Kupeana mali yao kama dhamana kwa wengine.
 • Tunahitaji kuomba sana kukanusha roho ya utoro, ufukara na upako wa utoro.

 

MWISHO

Omba:

 1. Nina vunja kila ngome ya utoro na upako wake Katika maisha yangu– katika Jina La Yesu Kristo.
 2. Nina vunja kila hali ya utumwa juu ya maisha yangu—Katika Jina la Yesu Kristo.
 3. Ee Bwana, panga maisha yangu kulingana na sababu zako kwangu, Katika Jina la Yesu.
 4. Ee Bwana, ufalme wako umiliki kila eneo katika maisha yangu– Katika Jina la Yesu.
 5. Bwana wangu, nina kataa kutumiwa ovyo-Katika Jina La Yesu.
 6. Bwana wangu , ninakataa maisha ya chini na kudharauliwa– Katika Jina La Yesu.
 7. Bwana wangu ninaomba kupenya kwangu katika kila eneo kufanyike sasa katika Jina la Yesu.

 

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *