Series Swahili Service WANAWAKE SABA WENYE IMANI YA BIBLIA

SARA– IMANI YA KUWA NA JAMII

SOMO:  YEREMIA 32:27,

               MWANZO 18:1-15

UTANGULIZI

Je,

ni jambo gani lililokupeleka mbali na Mungu wako. Mungu anataka wewe ufahamu kwamba yeye anayaweza yote,na sharti tumpe nafasi katika maisha yetu. Mungu atayabadilisha maisha yetu na kuyajibu maombi yetu. Katika Yeremia 32:27,  Mungu anawauliza waisraeli swali, “Tazama, Mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je kuna neno gumu lolote nisiloliweza?”. Mungu aliwauliza wana wa Israeli. Kila mmoja wetu anayeshida na kutoamini. Ibrahimu na Sara walimwomba Mungu kwa muda mrefu sana, miaka ikapita bila majibu. Pia wewe na mimi tunapata kugoja wakati unapita. Pengine ni shida ya nyumba yako, hau afya yako, watoto wako, kazi etc. Mungu yuasema, mambo mwanadamu hasiyoweza, Mungu anaweza (Luka 18:27). Kwa Imani Sara alipokea jamii, yeye aliyeitwa tasa aliyepitwa na wakati.

Hebu tutazame:-

I.   HOFU MBELE YA YASIYOWEZEKANA.

 • Tunaishi katika wakati gumu zaidi. 
 • Tunaishi katika magumu kiroho, uchumi, kanisa, jamii na taifa. 
 • Dunia nayo inayoshida– njaa, magonjwa, mauti, ukame, shida za serikali na shida za ndoa.
 • Watu wengi wamemsahau Mungu na kutafuta njia za mikato.
 • Watu wengi wamo tayari kuyauza maisha yao kupata wanayotaka.
 • Mfalme Yehoshapati alipata changamoto kuu, lakini alipomtazama Mungu na kukiri kwa hakuwa na namna, Mungu alimfungulia njia (2 Nyakati 20:1-4)
 • Wengi wetu hata ingawa tunaomba Mungu, hatumtengemei kamilifu, hivyo hatuoni mkono wa Mungu.
 • Mungu ni Mungu wa yasiyowenzekana– Mungu wa wote wenye mwili.

II.    IMANI INAYOONA YASIYO ONEKANA.

 

 • Imani yako ndani ya Mungu itakufanya kuona ukombozi wako, uponyaji wako, kuuishwa, Baraka na kibali chako. Hata kabla ya kupata unayo tarajia.
 • Hivi ndivyo Musa alivyoona katika Bahari ya shamu.
 • Hivi ndivyo mfalme Yehoshapati aliona aliposema “Vita ni vyake Bwana”
 • Mungu alimuuliza Yeremia, “Je kuna jambo?”
 • Mungu anafanya zaidi, juu ya yote (Waef. 3:20)
 • Je, ni afya yako– yeye ni tabibu, umasikini– yeye ni mwenye fedha zote (Hagai 2:8)

III. IMANI INAYOJARIBU YASIOWEZEKANA

 

 • Mungu alimtokea Sara alipokuwa na miaka 90.
 • Sara alicheka kwa kutoamini– Mungu alimkemea Sara (Mwanzo 18:14)
 • Baada ya miaka Mungu alimwambia Ibrahim amtoe Isaka sadaka (mwanzo 22:1-12)
 • Ibrahim aliamini Mungu wa ufufuo (Waebrania 11:19)
 • Yoshua naye, alisimamisha jua na mwezi mpaka vita vikamalizika (Yoshua 10:12-13)
 • Yesu Kristo aliingia Bethania– Lazaro akafufuka (Yohana 11:21)

 

MWISHO

 • Je, ni neno gani uliyonayo ndani ya maisha yako leo?
 • Shida yetu ni kukosa Imani.
 • Mjie mkombozi wako sasa

 

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *