Swahili Service

SAUTI YA VITA

I SAMWELI 11:1-15

UTANGULIZI

              Usipokimbia adui ataogopa sana kwamba wewe yuko tayari kwa vita, hivyo adui ndiye atakaye kukimbia. Ujumbe huu ni wa kutufundisha jinsi ya kupambana na nguvu zinazojivuna juu ya maisha yako (Dealing with boasting and proud powers of darkness). Ufalme wa mbinguni unaenda mbele kwa vita (Mathayo 11:12), Lazima kukabili adui na majivuno yake. Hebu tuone majivuno ya Nahashi, alipenda kufanya taifa yote ya  Israeli taifa la watu wa jicho moja. Ni jambo mbaya sana kuwa na adui husiyeweza kumshinda. Nahashi mfalme wa Waamoni alikuwa na nguvu nyingi sana. Alijua kwamba watu wa Yabesh-Gileadi hawakuwa na nguvu. Hata watu wa Yabesh– Gilead walijua hawakuwa na nguvu za kupigana na Nahashi. Hivyo, watu wa Yabesh-Gilead waliamua kufanya Amani na aduizao kwa mkataba. Shida tulionazo ni kwa sababu ya kufanya mikataba na adui zetu na marafiki na watu wa nyumba. Kuwaendea adui kutafuta msaada  kwa shida zetu ni hatia. Kutafuta msaada kwa adui dhidi ya adui nishida kubwa sana. (kama mama aliyekuwa na mtoto kiwete, mganga akaelekeza-mama mkwe, mama mkwe-amfungua mtoto, lakini watoto wao wote wakafa)Anaye kimbia ndiye anayefukuzwa (it is he who runs that is pursued ) (Zaburi 5:9 ; 120:7)

Hebu Tuone:-

I.    SHETANI ANAYO MASHARTI MBAYA (I Sam. 11:2)

 • Tunapo fanya mkataba wa Amani na shetani, lazima kutimiza masharti yake.
 • Shetani lazima kudharau Mungu wako na Imani yako.
 • Mtu anapokusukumia kuomba msaada kwa shetani, anataka heshima yako na ya Mungu wako kudharauliwa.
 • Nguvu na pepo za madharau wanajigamba jinsi wame haribu maisha ya watu wengi.
 • Pepo hawa wanataka kuonyesha Mungu hayuko pamoja nawe, wana funga kila njia ya msaada na yeyote anayetaka kukusaidia anaingia katika taabu nyingi sana.
 • Katika moto, watu wa Yabeshi-Gileadi walipokea usaidizi– Ni wakati wa Nahashi kushindwa leo.
 • Mungu anatuwacha kuingia motoni hili aingilie kati (Danieli 3:19-26)
 • Ahadi za Mungu tunapopitia majaribu (Isaya 43:2)

II.  NAHASHI ANATOKEA HILI IMANI YETU IPATE KUONEKANA

 1. Kudhibitisha kwamba adui yetu hana neno la mwisho juu yetu.
 2. Kukuza Imani yetu na ujasiri wetu dani ya Mungu (Shedrack, Meshack na Abednego)
 3. Kutufundisha masomo ya Imani na dhamana ya ukombozi.
 4. Kutuonyesha ya kwamba kuna nguvu ndani yetu. Mungu aliachilia Farao, Absaloni na Nebuchadnezzar hili nguvu zake zipate kuonekana.

III. JE, KUNAYE NAHASHI ANAYETAKA KUNG’OA MACHO YAKO ?

 • Wakati watu wameshindwa nawe, tumaini lako linapozimia, Mungu yupo.
 • Daktari anaposema ungojwa wako umeendelea Zaidi ya dawa.
 • Mungu si kiziwi kwa maombi yako.
 • Omba Mungu, tena lilia ukombozi wako, Nahashi wako lazima ashindwe.
 • Lazima pia huwe na hakika kwamba umeokoka.
 • Tubu kila dhambi unayoifahamu. Omba kujazwa na Roho Mtakatifu. Fahamu haki zako kama mtoto wa Mungu

 

MWISHO

Maombi

 1. Kila nguvu za giza zilizotumwa kunidharau– Kufa sasa Katika Jina La Yesu Kristo.
 2. Kila pepo aliyetumwa kujua na kupeleleza maisha yangu, sambaratika sasa Katika Jina la Yesu.
 3. Kila Goliathi na Farao katika hatima yangu, Kufa sasa katika Jina la Yesu.
 4. Milango yangu iliyofungwa na shetanui dhidi ya Baraka zangu– Funguliwa sasa Katika Jina La Yesu Kristo.
 5. Bwana wangu fanya nguvu za upepo, jua na mwezi kwenda kunyume na nguvu za shetani juu ya maisha na hatima yangu– Katika Jina la Yesu Kristo.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *