Swahili Service UKOMBOZI

SHINA LAKO LIKIUMIA

KUMBUKUMBU 29:18, MATHAYO 15:13      

UTANGULIZI         

Shina la kitu lina maana nyingi. Shina ni chanzo cha mtu hau kitu. Shina ni msingi, nanga, mwanzo hau katikati ya kitu hau mtu. Katika kumbukumbu 29:18, Bwana anasema kusiwe na mtu mume hau mke mwenye shina lizaalo uchungu na pakanga (wormwood). Uchungu ni sumu kali hau nyongo. Katika Warumi 11:16– kama shina ni takatifu mti ni takatifu. Shina linapokuwa mbaya, matunda yake  yana kuwa mbaya.(Kulikuwa na mwanamke msomi na tajiri, lakini aliabudu nyoka kwa siri. Nyoka alipokufa naye akafa, binti zake watatu waliokuwa wameshindwa ndoa walirudi kwa mume zao)

Hebu tuone:-

I.  SHINA NI NINI?

 • Shina hasa ni chanzo cha Mtu hau kitu.
 • Wazazi wetu ndio shina yetu, Upande wa baba na mama.
 • Kuokoka kunatupa ruhusa ya kupigana na mambaya ya nyumba tulipozaliwa na kuaibisha pepo za jamii.
 • Shida zetu zinaweza kuwa hadharani hau katika siri.
 • Kama jinsi shina la mti halionekani, hivyo shida nyingi hazionekani wazi.
 • Shetani anafahamu kwamba, shina la mtu linapoumia, matawi yake na matunda yake yatakuwa mbaya.
 • Adui anajua shina likiwa limeumia, basi hatima ya mtu (destiny) imo taabuni pia.
 • Adui anapo jeruhi shina, basi maisha ya mtu yameharibika.
 • Watu wengi wanakaa na majeraha makuu yaletayo sumu kali na pakanga.

II.  ISHARA ZA SHINA LILILOUMIZWA

 1. Kutokua katika Kristo na kukosa Baraka.
 2. Kutokujielewa mwenyewe (lack of self awareness)
 3. Kukataa miujiza ya Mungu katika maisha.
 4. Shida nyingi shuleni na kazini.
 5. Afya mbaya. Afya mbaya itamkosesha mtu hatima yake (Afya mbaya, umasikini na ujinga na kukataliwa vimbaya vinaenda pamoja).
 6. Kushindwa na dhambi haraka-kurudi nyuma na kukataa Neno.
 7. Maisha bila matunda ya Roho.
 8. Kuchanganyikiwa na maisha na frustration. (Mwanaume anataka kuwa mke, mke naye anataka kuwa mwanaume)
 9. Hofu na fadhaha, Tabia mbaya, tamaa ovu na kushindwa na majaribu.
 10. Kilio na maombolezo, kukata tamaa na kuvunjika moyo, kutoamini yeyote na kujificha watu.
 11. Uchungu na hasira, shida nyingi zaidi.
 12. Kutumiwa vimbaya na watu, umaskini, kutanga tanga, pepo za miamba, maji na za jangwa zinamfamia haraka. Shida za ndoa na jamii.

 

 

III. NGUVU ZINAZOCHANGIA;

 • Pepo zinazo mtesa mtu huyo zinaitwa pepo za mashinani.
 • Mababu wengine walichangia pakubwa. Hata mtu awe tajiri baadaye shida zitakuja.
 • Misingi duni inahitaji kuvunjwa katika Jina La Kristo Yesu.

IV.  JINSI YA KUTIBU SHINA LILILOUMIA,

 1. Tazama nyuma katika jamii na kuona shina zake.
 2. Tubu dhambi za jamii na kuomba Mungu akupasulie tawi lako.
 3. Anza vita juu ya pepo, omba Mungu nguvu.
 4. Toa maisha yako kwa Yesu Kristo na kumtumikia.

 

MWISHO

Omba:

 1. Kila pepo la kuharibu shina upande wa baba yangu shindwa katika Jina La Yesu.
 2. Kila pepo chafu upande wa mama yangu shindwa juu ya maisha yangu katika Jina La Yesu Kristo.
 3. Shina langu pokea uzima kwa njia ya moto katika Jina La Yesu Kristo.
 4. Ninavunja muungano wangu na pepo za ukoo na kabila langu, katika Jina La Yesu Kristo.
 5. Kila roho ya kuchelewa na kutoa na kunipunguza shindwa sasa katika Jina La Yesu Kristo.
 6. Roho wa Mungu tawala kabisa katika Jina La Yesu Kristo.

 

 

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *