Swahili Service

TENGENEZA MADHABAHU YA BWANA

I WAFALME 18:30-39

UTANGULIZI

Tunapotazama hali ilivyo katika kanisa mahali popote duniani leo, tunaona udhaifu, kutojitoa na kudidimia kwingi sana. katika makanisa mengi moto wa ufufuo na kuuishwa upya kumezimika kwa sababu dhambi, mwili na shetani amekolea sana. Shida si mchugaji hau ratiba ya kanisa. Shida hasa ni madhabahu yaliyovunjika katika maisha ya wateule wa Bwana. Sababu kuu ya madhabahu ni ibada, sadaka, matoleo,kusanyiko ya watu wa Mungu, kukutana na Mungu na kutengeneza agano na    Mungu. Madhabahu ni mahali pa kukutana; Mungu na mwanadamu, kukutana katika mwenye mwili na Roho Mtakatifu. Kila mtu aliyeokoka na asiye okoka anafahamu kwamba mambo ya Roho ndiyo yanasimamia mambo ya khadri (The Spiritual controls the Physical). Hivyo ndivyo wasio na Kristo wanatafuta sana kuwasiliana na nguvu za giza, hivyo wanaoga na sabuni maalumu na kujipaka manukato maalum hili kuvutia maroho kuwasaidia.

Madhabahu ni mahali pakukutana Roho na wenye mwili, iwe ni kukutana na Mungu wa Mbinguni hau shetani na mapepo. Hivyo ndivyo ilivyokuwa wakati wa Eliya, soma tena. Madhabahu ya Mungu yalikuwa yamefanywa madhabahu ya Baali.

Hebu tuone:

I.   SABABU YA KUTENGENEZA MADHABAHU YA BWANA.

 • Mungu anatukumbusha kujenga upya madhabahu yake hili naye amwage mapenzi, nguvu, ufufuo na uponyaji.
 • Roho mtakatifu anapotuleta mahali pa kujisalimisha katika nafsi zetu na katika mahali pa ibada mambo makuu yanafanyika katika kanisa la Bwana.
 • Sababu za kutengeneza madhabahu ya Bwana ni :
 1. Madhabahu ni mahali pa kujitoa (Consecration) na utakaso (Walawi 6:13)
 2. Madhabahu ni mahali pa kuungama na   kutubu dhambi (Isaya 59:2) uso wa Bwana  unafichwa na dhambi (Eze.39:29)
 3. Madhabahu ni mahali pa kunyenyekea.
 4. Madhabahu ni mahali pa kuomba (Mambo ya Nyakati 7:14)
 5. Madhabahu ni mahali pa kupokea ubatizo wa Roho mtakatifu (Yohana 7:37, Isaya 44:3)
 6. Madhabahu ni mahali pa uponyaji (Yakobo 5:14-16)
 7. Madhabahu ni mahali pa ibada na kuabudu Bwana (Zaburi 43:4, Zaburi 22:3)

II.  MASHARTI YA KUTENGENEZA MADHABAHU YA BWANA.

 1. utakatifu kama bibi harusi wa Bwana.
 2. Utii kwa Biblia kama neno la Mungu na usahihi wake.
 3. Ushuhuda wa wokovu kamili na ishara za kuokoka.
 4. Nidhamu ya kumpa Bwana heshima zote.
 5. Madhabahu ni lazima iwe ya Imani, sifa, shukrani na Ibada. ( Waebrania 11:6, Zaburi 65:1, 103:1-5, Zaburi 18:1-2)
 6. Madhabahu ni mahali pa maombi (Yeremia 33:3)
 7. Madhabahu yawe pahali pa kujitoa sadaka na dhabihu (2 Samweli 24:18-25, Warumi 12:1)

III. UFUFUO KWA KUTENGENEZA     MADHABAHU YA BWANA.

 • Tunachohitaji kama kanisa na Binafsi ni moto kutoka juu mbinguni ( I wafalme 18:36-37)
 • “Na ijulikane wewe ni Mungu” Mungu atajidhiriisha kuwa yeye ni Bwana.
 • Watu wa Mungu watamtafuta Bwana kwanza (Mathayo 6:33)
 • Eliya alikuwa mfano mwema kwetu ( Yakobo 5:17-18)

 

MWISHO

 • Je, unatafuta sana utukufu wa Mungu ?
 • Je, unatafuta sana Mungu apate sifa na Heshima ?
 • Wenye vita wa Bwana ndio mwenye ibada kwa Bwana.
 • Ni lazima kutenga hau kutengeneza madhabahu ya Bwana hili nguvu zake ziwe dhairi kwetu.
 • Lazima kuua ibada ya Baali katikati yetu.
 • Watu wa Mungu wataimba wimbo mpya “ Bwana ndiye Mungu, Bwana ndiye Mungu”.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *