Swahili Service

TUMEKOMBOLEWA TUKATUMIKE (SAVED TO SERVE)

LUKA 1:68-79

UTANGULIZI

Bethlehemu na Khaivari ni mahali pa mafundisho mengi. Pale Bethlehemu tunaona Neema ya Mungu, pale Khaivari tunaona chuki ya mwanadamu kwa Mungu muumba. Katika mlango huu tunaona nyimbo tatu.

 1. Wimbo wa Elizabeti (41-42)
 2. Wimbo wa Mariamu (46-55)
 3. Wimbo wa Zakaria (68-79)

Hebu tutazame wimbo huu wa Zacharia. Zacharia katika wimbo wake anatueleza kwamba tunaokolewa si hili tutosheke, kama vile hatuli chakula hili tushibe, bali tunakula hili tuishi, tupende na tufanye kazi. Hivyo tumekombolewa tuwezeshwe           kumwishia Mungu, tuwapende wezetu na kumtumikia Kristo.

Hebu tuone:-

I.  UKOMBOZI MKUU SANA (68-71)

 • Hapa tunakumbushwa kwamba, tumeokolewa kutoka kwa adui zetu.
 1. wokovu ni kwa Neema– ni kwa neema tu.
 • Tumeokolewa si kwa sababu ya matendo mema hau chochote ndani yetu. (Waefeso 2:8-10)
 1. Tumeokolewa kutoka kwa adui– Dhambi.
 • Dhambi ni adui mkuu wa nafsi zetu.
 • Mungu alitupa uhuru kutoka dhambini (Warumi 6:18)
 • Dhambi inatawala pasipo na wokovu (Warumi 6:14)
 1. Tumeokolewa kutoka adui– Mwili
 • Ubinafsi lazima ufe, Kristo aishi ndani yetu.
 • Wanaoishi katika mwili hawawezi kumpendeza.
 • Kwa Damu ya Yesu Kristo, ushindi unapatikana.
 1. Tumeokolewa kutoka kwa adui– Shetani
 • Mshitaki wetu ni Ibilisi
 • Lazima kuvaa silaha zote (Waefeso 6:11)

II.  SABABU YA UKOMBOZI (V.74)

 • Tunaokolewa hili tutumike (Warumi 6:18)
 • Tumeokoka hili tumwabudu Mungu bila hofu.
 1. Tumtumikie– Yeye pekee maana tunaye Bwana moja– Kristo.
 • Paulo alisema– Je nifanye nini Bwana,
 • Samweli alisema, Nena Bwana, mtumishi wako anasikia.
 1. Tumutumikie bila hofu.
 • Tumtumikie maana tunampenda– hakuna hofu katika pendo.
 • Tutmikie kama wana sikama watumwa (Warumi 8:15)
 1. Tumtumikie katika utakatifu.
 • Tumeitwa kwa mwito mtakatifu (2 Tim.1:9)
 • Yeye aliyetuita ni mtakatifu (I Petro 1:15)
 1. Tumtumikie katika haki ( Waefeso 4:24)
 2. Tutumike mbele zake
 • Tunatumika katika uwepo wake.
 • Elijah alitumika Mbele ya uwepo wa Mungu (I Wafalme 12:1)
 • Ibrahimu alitembea na Mungu.
 • Malaika Gabriel anatumika mbele ya uwepo wa Mungu (Luka 1:19)
 • Tunapotumika mbele ya Mungu hatutaogopa mwanadamu.
 1. Tumtumikie siku zote za Maisha yetu.
 • Hakuna kustaafu katika vita hizi.
 • Mlawi atastaafu baada ya miaka, lakini waliokombolewa na Bwana wanafanya kazi siku zote za maisha yao.
 • Siku zote za maisha ya utakatifu daima, milele.
 • Siku zote za maisha, hata katika udhaifu n uzee, siku zetu zote.

III. KAZI YA YOHANA MBATIZAJI (v.76-80)

 • Nabii wake aliye Juu.
 • Kutangulia mbele za uso wa Bwana.
 • Kutengeneza njia zake Bwana.
 • Kuwajulisha watu wake wokovu– msamaha wa dhambi zao.
 • Kuwajulisha kwamba mwangaza utokao juu umefika kwao.
 • Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti.
 • Kuongoza miguu ya watu kwenye njia ya Amani.

 

 

MWISHO

 • Tumeokolewa, tukatumike, Je, unatumika vipi?
 • Mwangaza kutoka juu umefika, Je umeupokea ?
 • Adui zetu wameshidwa, Je, wewe ushinda dhambi, mwili na shetani ?
 • Je, umeamua kumtumikia Bwana siku zote za maisha yako, hau unatumika kibarua ?

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *