Swahili Service UKOMBOZI

UKOMBOZI KUTOKA KWA FIMBO YA UDHALIMU

SOMO: ZABURI 125:1-5
ISAYA 14:1-5
UTANGULIZI

Mungu Baba anasema Fimbo ya udhalimu imekaajuu ya wenye haki kwa kitambo sasa. Lakini leo Mungu ataivunja hio fimbo ya uovu. Sababu, fimbo ya udhalimu ikikaa juu ya wenye haki, wenye haki watainyosha mikono yao kwenye upotovu !!. Hivi ndivyo wakristo wengi wanapo jaribiwa wanafanya mambo ya aibu. Unapoona watu wa heshima wanafanya mambo ya aibu, basi elewa fimbo ya udhalimu himo juu yao. Wanapo fanya aibu, basi haki yao inangeuka na kuwa  upotovu. Maombi yangu ni kwamba fimbo ya udhalimu (The rod of wicked) itavunjwa katika Jina la Yesu juu ya maisha yako.

Fimbo ya udhalimu pia inaitwa “gongo la wabaya” (Isaya 14:1-5) Fimbo ya udhalimu huja kwa vipimo (Size) na rangi nyingi, wakati waovu wanataka kuvunja mazuri ndani ya maisha ya wataule, Fimbo ya udhalimu na gongo la wabaya ndio ishara ya mamlaka ya waovu.Kwa wengine fimbo ya udhalimu inaanza mapema katika maisha.

Hebu tujifunze:-

I.  FIMBO NA GONGO YA WABAYA INAFANYA KAZI WAPI ?

 1. Fimbo hii inafanya kazi katika maisha yote
 • Hivyo hatima ya mtu inakuwa chini ya udhalimu na mabaya.
 • Waovu wanapo weka fimbo yao juu ya hatima ya mtu maisha yake yanakuwa magumu.
 • Maisha yake yanakuwa magumu hata kwa mambo ya kawaida.
 1. Fimbo ya udhalimu inatesa ndoa.
 2. Fimbo ya udhalimu inaua maono ya mtu (Vision and plans)
 3. Fimbo ya udhalimu inaingilia biashara na kazi ya wenye haki.
 4. Fimbo ya udhalimu inashambulia afya ya kizazi, mikono, miguu na mioyo ya wenye haki.
 5. Fimbo ya udhalimu inachangia upunguvu wa Baraka, huku fimbo hii inaongoza mtu katika njia kinyume (frustration) maisha yake yanakuwa ngumu. Kitu kinacho chukua siku kinafanyika baada ya miaka. Baadaye mauti.

II.  JE FIMBO YA UDHALIMU INAWEKWA LINI?

 • Wakati nyota yako imeng’ara.
 • Wakati mambo yako yanaendelea vyema.
 • Wakati tumaini lako liko juu Zaidi na shabaha zako zimefikiwa.
 • Wakati umepenya katika maisha.
 • Wakati unasema sasa ninaweza kustarehe kwa kazi yangu.
 • Wakati unasema sasa hamna shida nimeitimu Zaidi, wakati madaraka yameingia.

III. BASI TUFANYE JE ?

 • Wakati fimbo inafanya kazi, mtu anakasirika bure, wakati tunaanza kutumia hekima ya dunia (Isaya 60:18-19)
 1. Jua kwamba Mungu pekee ndiye Mkombozi
 2. Kama ujaokoka-mlilie Bwana akuokoe.
 3. Tafuta sana kutembea na Mungu wako.
 4. Kata kiburi ndani ya maisha yako.
 5. Mwite Bwana kwa ukombozi kutokana na fimbo ya udhalimu na gongo la ubaya.

 

MWISHO

Omba:

 1. Kila fimbo ya udhalimu na gongo la ubaya katika jamii yangu, pokea moto wa Mungu, chomeka mpaka jivu Katika Jina la Yesu Kristo.
 2. Wewe nguvu za fimbo dhidi ya maisha yangu pooza sasa katika Jina la Yesu kristo.
 3. Damu ya Yesu Kristo nikomboe katika Jina La Yesu Kristo
 4. Fimbo ya udhalimu achilia ndoa yangu, afya yangu, kizazi changu, utukufu wangu na Baraka zangu, katika Jina La Yesu Kristo.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *