Swahili Service

“ULIZENI HABARI ZA MAPITO YA ZAMANI”

YEREMIA 6:16

UTANGULIZI

Katika siku hizi msafiti wa kiroho anafika katika njia panda. Hivyo kuna sababu ya kusimama, kuona na kuuliza “I wapi njia iliyo njema?”. Kwa maana njia ni nyingi siku hizi. Lakini njia ya Mungu na zamani ni moja, wengine walipita njia hio na wakafika (Waebrania 11: ). Leo ni Jumapili ya Mwisho wa mwaka 2018. Bwana amekuongoza majuma 52 mwaka huu. Leo ni siku ya shukrani kuu, huku tukitazama mbele, kwa mwaka kesho yaani 2019. Basi ujumbe wa leo unatuelekeza mbele.

Hebu tujifunze:-

I.  KWANINI KUULIZA MAPITO YA ZAMANI?

 • Kwa sababu njia mpya ni potovu na ndanganyifu sana.
 • Njia mpya ni njia ya mwanadamu na ni kinyume na njia kuu ya Bwana (Isaya 35:8)
 • Njia na mapito ya zamani ni njia ya utakatifu.
 • Wasio safi hawatapita juu yake.
 • Hii ni njia ya wasafirio, wajinga wanapotea njia hii ya utakatifu.
 • Hii njia haina simba, wala wanyama wakali,
 • Hii ni njia ya walio kombolewa na Bwana wao.
 • Basi nawe ukasimame, ukatazame, ukaulize hii njia ya zamani.

 

II.   JE, NJIA NA MAPITO YA ZAMANI NI NINI HASA?

 • Mapito ya zamani walipita, habeli, Ibrahimu, Musa, Daudi, Elija , manabii na Mitume wa Kristo.
 • Hawa walimwamini Mungu, walipokea neno lake kuwa nuru na mwangaza kwa muguu yao.
 • Ushuuda wa Kristo ulikuwa msingi imara na tumaini lao.
 • Hawa walifuata ufunuo wa Mungu na mapenzi yake mpaka wakaingia paradizo yake Mungu.
 • Mapito ya zamani yamenyunyiziwa damu ya Mwana Kondoo wa Mungu.
 • Mapito ya leo na sasa yamepakwa mafuta na maji ya kumpendeza mwanadamu.

III. KWANINI TUPITIE MAPITO YA           ZAMANI?

 • Tunapitia mapito ya zamani kwa sababu hapa tunapata:
 1. Damu ya Yesu Kutuhesabia Haki.
 • Wasafiri wote, wanaopita mapito ya zamani wamesamehewa na kuhesabiwa haki kupitia damu ya Yesu Kristo na Msalaba wake.
 • Wanao safiri katika mapito ya sasa hawajui mambo ya damu na utakaso wa Bwana.
 1. Neno la Bwana Inawatosha
 • Hawa wapitao mapito ya zamani hawawezi kukimbilia hadithi za mwanadamu.
 • Hawa wapitao mapito ya zamani wanafahamu kwamba ushuhuda wa Yesu Kristo ndio Roho ya Unabii.
 • Hadithi za mwanadamu na shuhuda zao haziwezi kutuliza na kutoshelesha mahitaji ya moyo na matumaini ya mwanadamu.
 1. Nguvu za Roho Mtakatifu Kutakasa
 • Mapito mpya hayawezi kubadilisha maisha kwa sababu Mungu hawezi kuruhusu mambo yasio kweli kutosha na kutuliza mioyo ya mwanadamu.
 • Mapito ya zamani ni mapito ya Amani, furaha, upendo na nguvu za    Mungu.
 • Mapito ya zamani ni mapito ya Kristo na Roho Mtakatifu.
 • Tunapopita mapito ya zamani tutajipatia Raha Katika nafsi zetu.

 

 

MWISHO

 • Wao wa wakati wa Yeremia walisema, “Hatutaki kwenda katika njia hiyo”
 • Mungu aliwaambia wasikilize sauti ya tarumbeta yake– Lakini walisema “ Hatutaki kusikiliza”.
 • Lakini hivi leo, wewe pamoja nami tunasema nini?

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *