Swahili Service UKOMBOZI

WIMBO WA MUSA NA WIMBO WA MWANA KONDOO

ISAYA 51:11

KUTOKA 15:1-19   

UTANGULIZI

“Nao waliokombolewa na Bwana watarejea, watafika Sayuni, wakiimba; Furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao, watapata shangwe na furaha, Huzuni na kuugua zitakimbia.”

Hapa Biblia inaongea juu ya wimbo wa Musa na wimbo wa Mwana Kondoo. Hebu tuone wimbo wa Musa unaimbwa na nani, ni nani anastahili kuimba wimbo huu?. Soma tena Kutoka 15:1-19, Wimbo wa Musa unasema Yakobo alienda Misri kutoka Kanaani kwa sababu ya njaa, wana wa Israeli walikuwa Misri miaka 430 katika hali ya utumwa. Kwa nini Mungu aliwaweka Misri miaka mingi hivyo ?

Tazama (Mwanzo 46:5-7) na (Mwanzo 15:12-15), maelezo ya safari na utumwa Misri.

 1. Wale waendao Mbinguni lazima kwanza wawe wageni na wasafiri hapa duniani. Bila utumwa hatuwezi kuelewa uhuru.
 2. Waendao mbinguni lazima kupita Misri– Misri maana yake ni ulimwengu. Kila aliyeokoka lazima kuhama Misri.
 3. Wamisri lazima kuwatesa wanaombaki Misri na kucheza wimbo wao ni mateso Zaidi
 4. Mungu alipenda wana wa Israeli wapitie wakati wao wa mitihani.

Hebu Tuone:-

I.    SHULE ZA MUNGU

 • Sasa hii wengi wetu wanapita katika shule ya Mungu. Wengi hawajui kwa nini wapite.
 • Shule ya Tabia Nzuri- Tabia ni jambo la maana sana. Tutaenda mbinguni na tabia zetu. Lazima kupita mtihani wa tabia nzuri na  nidhamu.
 • Shule ya unyenyekefu na upole– Mungu anapoona kwamba umekosa unyenyekefu atakufanya kutumika chini ya wandogo wako.
 • Shule ya Kiasi: -Wengi wamekuwa bila kiasi kwa muda mwingi, sasa Mungu anawafundisha self-control (Kiasi)
 • Shule ya Maombi: -Mitihani yetu inatufanya kuomba sana na kukesha.
 • Shule ya kufunga saumu: -Pengine ulipewa na Mungu kipawa, fedha, mali, lakini ukatumia vimbaya. Sasa ni kufunga na kuomba Mungu akupatie nafasi ya pili.

Yesu Kristo kama Mwana wa Mungu alipitia katika shule za Baba ajifunze utii.

 • Wengi wetu hatuwezi kuimba wimbo wa ushindi leo kwa maana tungaliko Misri bado.
 • Wimbo wa Musa ni wimbo wa ushindi.
 • Walimshinda Farao, walivuka bahari ya shamu, waliona ushindi wa Bwana.
 • Wimbo wa Musa ni wimbo wa walio panda milimani na mabonde, bahari na askari wa Farao.
 • Wimbo wa Musa ni wimbo wa “Zaidi ya washindi”.
 • Kristo hapendi yeyote kuishi katika utumwa wa Misri. Hivyo tumia binu za Musa kujipatia ushindi. Watumie adui zako moto, tauni, shinda, damu.
 • Mpaka adui anapoangamia baharini ndio wimbo wa Musa utakapoimbwa.

II.  NYIMBO NI MBILI.

 • Wimbo wa Musa ni wimbo wa kwanza, wimbo wa Musa ni wa ushindi wa kwanza. (Initial victory)
 • Ushindi wa kwanza ni ushindi juu ya shetani na mwili. Lakini ushindi huu wa kwanza hautoshi.
 • Ushindi wa mwisho ni bora zaidi, wimbo wa Mwana Kondoo.

III. WIMBO WA MWANA KONDOO (Ufunuo 15:3-4)

 • Wimbo wa mwana Kondoo ni wimbo wa waliokombolewa- wanaofika Mbinguni.
 • Kila mtu huko mbinguni ni mwimbaji.
 • Ni jambo mbaya wengi wa walio kanisani hawaendi mbinguni, maana wakosa kuacha Misri.
 • Wengine wametupa talanta zao hivyo hawatumiki.
 • Wengi hawapendi injili ya Kristo na hawapendi kuwatagazia wengine habari njema.
 • Wengine wako katika shule ya Yona– Wasiotii.
 • Wengine wanakaa katika ndoa zizizo za kibiblia.
 • Hawawezi kuimba wimbo wa Musa na Mwana Kondoo.
 • Ili Mtu kuimba wimbo wa Musa lazima uwe huru kutokana na kiburi , tamaa mbaya na chuki.

MWISHO

Omba:

 1. Kila huzuni na kuugua kimbia kutoka kwangu kwa moto katika Jina La Yesu.
 2. Kila nguvu zinazo ni nyima ushindi wangu toweka katika Jina la Yesu.
 3. Ninatangaza upepo, gurumo na umeme wa Roho Mtakatifu dhidi ya adui na ngome zake– Katika Jina La Yesu Kristo.
 4. Ninalowesha maisha yangu, jamii na chochote katika Damu ya Yesu Kristo.
 5. Bwana wangu nibatize katika haki na moto katika Jina La Yesu.
 6. Kila nguvu inayoiba mali yangu, anguka na kufa katika Jina La Yesu.
 7. Wewe roho wa mauti juu ya maisha yangu, kila mpango wa shetani juu ya maisha yangu, Shindwa katika Jina La Yesu Kristo.
 8. Ninaamurisha kila laana, pepo za ukoo, kila ulimi, shindwa katika Jina La Yesu.
 9. Bwana wangu ninajiweka bali na kila sanamu, pepo za jamii, madhabahu ya shetani, ushirika mbaya ,tamaa mbaya na ibada za shetani, katika Jina La Yesu Kristo.
 10. Baba yangu ninakushukuru kwa ushindi wako katika Jina la Yesu Kristo

AMEN

 

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *